Anthony Joshua 'arudi ulingoni' baada ya ajali
Fury na Joshua wamekaribia kuzipiga kwa mara ya kadhaa, lakini majadiliano hayakuwahi kufanikiwa kipindi chote.
Tyson Fury anatarajiwa kupambana na Anthony Joshua baadaye mwaka huu, kulingana na ‘promota’ wa masumbwi Spencer Brown, ambaye anasimamia uwezekano wa Fury kurudi kuzipiga dhidi ya Arslankbek Makhmudov.
Brown aliiambia Sky Sports kuwa pigano hilo kati ya mabingwa wa uzani wa juu raia wa Uingereza huenda likafanyika, iwapo Fury atamshinda Makhmudov.
"Ndondi sasa hivi iko pazuri," Brown aliiambia Sky Sports. "Itakuwa jambo la kufurahisha sana. Itakuwa Kombe la Dunia la ngumi kwangu.
"Tumetaka hili lifanyike kwa muda mrefu, sasa wakati umefika… nadhani hivyo."
Majadiiliano hayakufanikiwa
Kwa mara ya kadhaa Fury na Joshua walikuwa wapambane, lakini majadiliano hayakufanikiwa kutokana na utata wa mkataba, wasiwasi kuhusu utayari, na kushindwa.
Timu zao zilikuwa ziko karibu kufikia makubaliano kabla ya Joshua kujiondoa kwenye masumbwi kwa muda kufuatia ajali ya gari Disemba ambayo ilisababisha vifo vya marafiki zake wawili na mkufunzi.
Joshua mwenye umri wa miaka 36 ameanza mazoezi na alikuwepo kwenye pambano la Jumamosi ambapo Derek Chisora alishindwa na Deontay Wilder.
"Sidhani kama linatakiwa kuwa pambano linalofuata kwa AJ baada ya kile kilichotokea na alichokiona," Brown alisema.
"Nadhani ana maamuzi mawili. Apigane pambano la awali. Inabidi apate mpinzani sahihi.