Jeshi la Guinea-Bissau lasema limetibua jaribio la mapinduzi lilohusisha maafisa kadhaa
Maafisa waliokamatwa kwa madai ya kuhusiska na jaribio hilo, wanahojiwa kwa sawa, naibu mkuu wa majeshi amesema
Jeshi la Guinea-Bissau limetangaza kuwa lilitibua jaribio la mapinduzi siku ya Ijumaa lilohusisha maafisa kadhaa, kulingana na vyombo vya habari.
Majenerali wa jeshi wamejitokeza katika mkutano na waandishi wa habari mubashara na kushtumu “jaribio linginge na kukiuka utaratibu wa katiba” kabla ya uchaguzi ulioratibiwa kufanyika Novemba 23.
Naibu Mkuu wa Majeshi Jenerali Mamadu Ture amesema uchunguzi unaendelea na wote waliohusika watakamatwa, Shirika la habari la Guinea-Bissau, Capital News limeripoti.
Maafisa kadhaa wamekamatwa katika siku za hivi karibuni, ikiwemo mkuu wa chuo cha kijeshi huko Cumere, Jenerali Daba Na Walna, kwa madaia ya kuhusika na jaribio la mapinduzi.