Urusi na Ukraine zabadilishana miili ya wanajeshi waliouawa vitani

Kufikia sasa, Ukraine imepokea jumla ya miili 1000

By
Jumla ya wafungwa 1,800 wa Kirusi walirudishwa nchini mwao mwaka 2025, kulingana na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu./Picha:@TRTWorldNow

Urusi na Ukraine zimekabidhiana miili ya wanajeshi waliouwawa kwenye vita baina ya nchi hizo.

"Urusi imekabidhi miili ya wanajeshi 1,000 wa Ukraine waliouwawa, huku nayo ikipokea miili 35,” ilisema Urusi kupitia jukwaa la Telegram.

Hatua hiyo, inafuatia makabidhiano ya awali ya miili hiyo, iliyofanyika Januari 29.

Toka kuanza kwa vita hivyo, Urusi na Ukraine zimekuwa zikibadilishana wafungwa.

Jumla ya wafungwa 1,800 wa Kirusi walirudishwa nchini mwao mwaka 2025, kulingana na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu Tatyana Moskalkova.