Zimbabwe imekumbwa na hitilafu kubwa ya umeme na kusababisha nchi nzima kuingia gizani siku ya Jumatatu.
Tatizo hilo la umeme lilianza kuripotiwa mida ya jioni, kulingana na Shirika la Umeme la nchi hiyo (ZETDC).
"Idara zote zimefahamishwa kuhusu tatizo hilo na jitihada zinaendelea kuweza kutatua changamoto hiyo," ilisomeka sehemu ya taarifa ya ZETDC.
ZILIZOPENDEKEZWA
Hata hivyo, kampuni mama ya umeme nchini humo (ZESA), ilisema kuwa changamoto hiyo ilitokana na hitilafu, ikiongeza kuwa mafundi walikuwa kazini kuhakikisha hali ya kawaida inarejea.
Zimbabwe imekumbwa na hitilafu za umeme kutokana na uzalishaji mdogo wa nishati hiyo na kuzeeka kwa miondombinu ya uzalishaji.
CHANZO:AFP
















