Elia Mpanzu aongeza mkataba wa miaka miwili Simba Sports Club
Mchakato huo unatajwa kufanikishwa na rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji.
kNyota wa kimataifa kutoka DRC anayechezea Simba Sports Club ya Tanzania, amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea klabu hiyo, Machi 23, 2026.
Mchakato huo unatajwa kufanikishwa na rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji.
Mpanzu aliyejiunga na ‘Mnyama’, Septemba 2024, aliwahi kuhusishwa kujiunga na mahasimu wa jadi wa Simba, Young Africans.
Wachambuzi wa soka nchini Tanzania, wanaamini kuwa Mpanzu akiwa katika hali ya utulivu wa kiakili, uwezo wake halisi huonekana zaidi uwanjani—hali ambayo ni habari njema kwa mashabiki na benchi la ufundi la Simba.
Toka ajiunge na ‘Wekundu wa Msimbazi’, Mpanzu amefumania nyavu mara 29, na kutoa pasi za usaidizi (assists) 10.