Hivi karibuni Marekani ilitia saini makubaliano ya ushirikiano wa nishati ya nyuklia na Saudi Arabia, yaliyoelezwa na Wizara ya nishati ya Marekani kuwa “ya kihistoria”.
Waziri wa Nishati Chris Wright na Waziri wa Nishati wa Saudi Arabia Mwanamfalme Abdulaziz bin Salman walitia saini makubaliano kifungu cha 123 chini ya Sheria ya Nishati ya Atomiki, kikichagizwa na makubaliano ya pande zote mbili.
Hata hivyo, makubaliano hayo yamesababisha mjadala mkali kwa sababu yanadaiwa yanaruhusu Saudi Arabia kurutubisha madini ya urani, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Hali kama hii imewahi kuwepo katika kanda hiyo, isipokuwa wakati huu muktadha na maelezo yake ni tofauti.
Iran na neno N
Kwa karibu miongo miwili, mfumo mzima wa mpango wa nyuklia wa Iran ulikuwa na mtazamo kama Iran ni tatizo ambalo linatakiwa kutatuliwa kivyake. Lakini hali haikuwa hivyo.
Israel imekuwa na silaha za nyuklia ambazo haijaweka wazi kwa miongo kadhaa.
Mataifa ya Ghuba yana wasiwasi wao kuhusu usalama wa muda mrefu kabla ya tatizo la sasa na Iran na wasiwasi huo utakuwepo hata baada ya makubaliano haya.
Hali hii ya kuona mpango wa kurutubisha wa Iran kama ukiukwaji ndiyo iliosababisha ubaguzi tunaouona hii leo.
Muundo wa usalama uliofanya nchi moja kuwa agenda, na kutozingatia masuala mengine, kusingewezekana kuendelea. Ilikuwa ni hatua ya muda tu.
Kuiwekea vizuizi nchi moja wakati ukiipa silaha nyingine ni sera ya kibaguzi.
Ndiyo sehemu hii ya makubaliano ya Saudi Arabia ambayo imekosolewa zaidi.
Wiki iliopita, Rais wa Marekani Donald Trump aliandika katika mtandao wa kijamii wa Truth Social kuwa "hakutakuwa na urutubishaji," akisisitiza kuwa Saudi Arabia itapokea tu “malighafi ambazo hazitakuwa na kurutubisha nyuklia”.
Hata hivyo, taarifa rasmi kutoka Wizara ya Nishati ya Marekani haizungumzii suala la urutubishaji wa urani kabisa.
Seneta Ed Markey tayari amewasilisha sheria ya 'Hakuna Silaha za Nyuklia kwa Saudi Arabia', ambayo inataka Saudi Arabia kuachana rasmi na mpango wa kurutubisha urani.
Ni wazi kuna undumakuwili: taifa moja linaweka vikwazo dhidi ya lingine kwa muongo, hadi kulishambulia taifa moja, kuhusu mpango wake wa kurutubisha urani.
Alafu mamlaka hizo zinajadili fursa kama hizo za kurutubisha taifa lingine kwenye kanda hiyo hiyo — Siyo tena suala la msingi, lakini la upendeleo.
Kila nchi jirani inaona. Na kila mtu anakumbuka hilo.
Kipi kinachofuata kwa Iran?
Kwa miaka mingi, mjadala kimataifa umekuwa ni: “Iran itatengeneza bomu la nyuklia?"
Swali lilikuwa linalenga mpango wa Iran.
Hata hivyo, kuibuka kwa mpango wa urutubishaji wa urani wa Saudi Arabia – hata kama rasmi unaelezwa kuwa ni kwa raia tu – unabadilisha swali ambalo Iran yenyewe inajiuliza hadi leo.
Swali sasa siyo kama Iran iendelee kuwekewa vikwazo, lakini ni kwa nini Iran itakiwe kuwa na vikwazo ambavyo mahasimu wake upande wa pili wa Ghuba ya Basra hajawekewa.
Haya si mabadiliko ya mawazo. Saudi Arabia tayari imetia saini makubaliano ya kijeshi ya silaha za nyuklia za Pakistan. Makubaliano hayo yalikamilia mwaka uliopita baada ya mashambulizi ya Israel nchini Qatar kuyafungua machi mataifa ya Ghuba.
Baada ya hapo, hata Waziri wa Ulinzi wa Pakistan alieleza kuwa uwezo wa nyuklia wa Pakistan "utapatikana" kwa Saudi Arabia kama utahitajika. Matamshi haya yalitafsiriwa kote katika kanda kama yalivyokusudiwa.
Mwanamfalme kiongozi Mohammed bin Salman amekuwa akisema mara kwa mara kuwa Saudi Arabia itatengeneza silaha zake za nyuklia iwapo Iran itapitiliza mipaka kuhusu nyuklia.
Uturuki, ambayo imekuwa na mkakati wake wa nyuklia kwa ajili ya raia na wasiwasi wa usalama wake kwa eneo ambalo limekuwa na hali tete, haiwezi kukaa kimya na kuangalia tofauti hizi kama jambo la kupita.
Kinachoonekana ni mabadiliko ya uwezo katika kanda. Hili halifanyiki kupitia mifumo ya kimataifa iliyokubaliwa, bali kupitia makubaliano ya mataifa. Hili ndilo linalofanya hali kuwa tete zaidi.
Hapa ndipo mtazamo wa Uturuki ulipotumika — na kuonekana kufanya kazi zaidi.
Mei 2010, Uturuki na Brazil walifanya kitu ambacho hakuna mfumo wa kimataifa uliowahi kufanya jambo hilo wakati huo.
Wakishirikiana na Iran moja kwa moja, aliyekuwa waziri mkuu wa Uturuki wakati huo ambaye sasa ni Rais Recep Tayyip Erdogan na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva walianzisha kile kilichojulikana kama Azimio la Tehran.
Chini ya mpango huo, Iran ilikubali kuhamisha kilo 1,200 za urani yake iliyorutubishwa hadi Uturuki ili wapate mafuta ya nyuklia kwa ajili ya utafiti.
Makubaliano yalikuwa ya kimsingi, ambapo mataifa ya P5 hayakukubaliana nayo.
Iran, kama wengine ina haki ya kuwa na teknolojia ya nyuklia ya amani. Kuaminiana kunaweza kujengwa siyo kwa vikwazo na vitisho.
Marekani na washirika wake waliona makubaliano hayo kama yasiyoridhisha, na baada ya siku chache, kuweka vikwazo vingine.
Hata hivyo, hekima ya mtazamo wa Uturuki ilikuwa wazi wakati huo — na ina umuhimu zaidi hata leo.
Matatizo ya nyuklia katika kanda yameongezeka, hatari zaidi pale yanapoangaziwa kwa shinikizo na makubaliano yanayoegemea upande fulani, yakitafsiriwa tofauti na nchi mbalimbali kutokana na maslahi ya nchi hizo.
Yanakuwa thabiti wakati kanda nzima inajumuishwa katika mfumo mmoja ambao unaweza kuthibitishwa na wote na kuonekana kuwa wa haki kwa wote. Miaka kumi na tano iliopita, Uturuki ilieleza sababu hizi kuhusiana na Iran.
Leo hii, ni muhimu kurudia — safari hii kwa Marekani na Saudi Arabia – kabla sheria hizi kubadilisha kabisa muelekeo kwa waangalizi wote.
(Makala haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza na TRT Russian)




















