| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Rais wa Niger Tchiani aanza ziara ya kikazi nchini Uturuki
Rais wa Niger anaanza ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa Rais mwenzake wa Uturuki.
Rais wa Niger Tchiani aanza ziara ya kikazi nchini Uturuki
Rais Abdourahamane Tchiani amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan, wa Ulinzi Yaşar Güler na wa Nishati Alparslan Bayraktar. / AA

Rais wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani, amewasili nchini Uturuki siku ya Jumatano usiku kuanza ziara rasmi ya kikazi.

Katika taarifa iliyotolewa na serikali ya Uturuki inaeleza kuwa kiongozi huyo wa Afrika Magharibi anafanya ziara kwa mwaliko wa Rais mwenzake wa Uturuki.

"Kupitia mwaliko wa Rais Recep Tayyip Erdoğan, Rais wa Jamhuri ya Niger, Abdourahamane Tchiani, atafanya ziara ya kikazi nchini Uturuki Juni 4, 2026," alieleza Burhanettin Duran, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa serikali ya Uturuki, katika ujumbe kwenye mtandao wa X.

Taarifa hiyo iliongeza, "Wakati wa mazungumzo, masuala yote ya uhusiano wa mataifa mawili kati ya Uturuki na Niger yatatathminiwa, na hatua zaidi za kuimarisha ushirikiano zitaangaliwa tena."

Ziara muhimu

Taarifa hiyo ilieleza pia, "Viongozi hao wawili watajadili masuala ya kikanda na yanayojiri duniani kwa sasa."

Katika taarifa nyingine siku ya Jumatano, ofisi ya Rais wa Niger imethibitisha kuwa Rais Tchiani ameondoka kuelekea Uturuki "kwa ziara ya kikazi na ushrikiano yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili."

Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa maafisa kadhaa waandamizi wa Niger wanaoongozana na Tchiani kwenye ziara hiyo, ikifafanua kuwa wote wana majukumu muhimu ya maendeleo kwa taifa.

Ilieleza kuhusu nafasi za mawaziri walio kwenye ujumbe huo zinaonesha dhamira ya mamlaka za Niger katika kuimarisha ushirikiano na Uturuki kwenye sekta mbalimbali ambazo zinaonekana kuwa za kipaumbele kwa uchumi wa Niger, viwanda na usalama.

Maafisa hao waandamizi wa Niger kwenye ujumbe wanajumuisha: Jenerali Salifou Mody Waziri wa Ulinzi, Garba Hakimi Waziri wa Afya, Salissou Mahaman, Waziri wa Miundombinu, Ousmane Abarchi, Waziri wa Madini.

Wengine kwenye ujumbe huo ni pamoja na Bakary Yaou Sangaré Waziri wa Mambo ya Nje, Soumana Boubacar Mkuu wa Utumishi wa Umma na Msemaji wa Serikali, Maman Laouali Abdou Rafa Waziri wa Fedha, Mahaman Elhadj Ousmane Waziri wa Kilimo, Amadou Haoua Waziri wa Nishati, Abdoulaye Seydou Waziri wa Biashara na Viwanda na Salou Adama Gazibo Balozi wa Niger nchini Uturuki.

CHANZO:TRT Afrika English