| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Jeshi la Somalia lawaua magaidi wa Al Shabaab wakiwa katika mkutano wa kupanga mashambulizi
Operesheni hiyo ililenga viongozi wa Al Shabaab katika eneo la katikati mwa Shabelle, na baadhi yao waliuawa, anasema waziri wa habari.
Jeshi la Somalia lawaua magaidi wa Al Shabaab wakiwa katika mkutano wa kupanga mashambulizi
Vikosi vya Somalia vimekuwa vikikabiliana na magaidi kwa miaka kadhaa. / AA
tokea masaa 13

Idsra ya Ujasusi ya Somalia (NISA) inasema kuwa Jumapili ilifanya operesheni dhidi ya kundi la kigaidi lenye uhusiano na Al Qaeda la Al Shabaab, na kuwaua wanachama wake 13, ikiwemo viongozi wake watano.

Operesheni hiyo ilifanyika katika eneo la Maha Saed katikati mwa Shabelle, ikilenga mkutano wa viongozi wa Al Shabaab.

“Viongozi hawa makatili waliolengwa walikuwa wanafanya mkutano wa kupanga njama ya mashambulizi ya kigaidi na kuweka shinikizo kwa jamii kuwaunga mkono. Hata hivyo, maafisa wa kijasusi walifanikiwa kuzima njama zao baada ya kukabilia wakiwa kwenye kikao chao,” NISA ilisema kwenye taarifa.

Shirika hilo liliwataja viongozi hao waliouawa kuwa ni Moalim Aseyr, Moalim Muhumed Ahmed Hassan, Sheikh Ali Guuraale, Abdirahman Sheikh Ali Dhegey, na Moalim Adey.

Operesheni mahsusi

Inasema kuwa walikuwa wanahusika na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika eneo la katikati mwa Shabelle, Galgaduud, na Bay.

“Hadi wanachama wanane, ikiwemo viongozi watatu, pia walijeruhiwa vibaya katika operesheni hiyo.

Operesheni ilitatiza mipango ya kigaidi katika mikoa mitatu, kulingana na Waziri wa Habari wa Somalia Daud Aweis.

Kundi hilo la kigaidi lenye uhusiano na Al Qaeda limekuwa likikabiliana na serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 16, mara nyingi likilenga maafisa wa usalama, wa serikali, na raia.

Tangu Julai mwaka uliopita, jeshi la Somalia, kwa msaada wa majeshi ya Umoja wa Afrika na washirika wa kimataifa, limeimarisha operesheni zake dhidi ya Al Shabaab.

Vikosi hivyo vya AU viliongezewa muda wa mwaka mmoja zaidi na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hadi Disemba 31.

CHANZO:AA