| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Rais Erdogan atuma rambirambi kwa watu wa Azerbaijan wanaoadhimisha miaka 34 tangu mauaji ya Khojaly
“Hatutasahau kamwe mauaji haya ya kinyama, ambayo maumivu yake tutayahisi daima katika mioyo yetu,” amesema Rais wa Uturuki Erdogan.
Rais Erdogan atuma rambirambi kwa watu wa Azerbaijan wanaoadhimisha miaka 34 tangu mauaji ya Khojaly
Rais Recep Tayyip Erdogan aliadhimisha kumbukumbu ya miaka 34 ya Mauaji ya Khojaly. / / AA
26 Februari 2026

Rais wa Uturuki ametuma salamau za rambirambi kwa raia ndugu wa Azerbaijan kufuatia kumbukumbu ya miaka 34 tangu mauaji ya Khojaly.

“Katika kumbukumbu ya miaka 34 ya mauaji ya Khojaly, ninawakumbuka kwa rehema na huzuni ndugu zetu wa Azerbaijan waliouawa kishahidi, na ninatoa pole zangu kwa ndugu na rafiki zetu wa Azerbaijan,” Erdogan amesema katika ujumbe uliouchapisha kwenye jukwaa la mitandao ya kijamii la NSosyal nchini Uturuki.

Mauaji ya Khojaly

Muda mfupi baada ya kuvunjika kwa Muungano wa Kisovyeti, vikosi vya Armenia viliteka mji wa Khojaly katika eneo la Karabakh tarehe 26 Februari 1992, baada ya kuushambulia kwa mizinga mizito na vifaru.

Mji huo ulishamabuliwa kwa saa mbili na vikosi vya Armenia, ambapo raia 613 wa Azerbaijan waliuawa, wakiwemo wanawake 106, watoto 63 na wazee 70, huku wengine 487 wakijeruhiwa vibaya, kwa mujibu wa takwimu za Azerbaijan.

Takriban watu 150 kati ya Waazerbaijan 1,275 waliotekwa wakati wa mauaji hayo bado hawajulikani walipo hadi leo, huku familia nane zikiripotiwa kumalizwa kabisa.

Eneo la Karabakh lilishuhudia mauaji ya halaiki na mazishi ya pamoja wakati wa Vita ya Kwanza ya Karabakh mwanzoni mwa miaka ya 1990, ambapo vikosi vya Armenia vilichukua udhibiti wa Nagorno-Karabakh — eneo linalotambuliwa kimataifa kuwa sehemu ya Azerbaijan — pamoja na maeneo saba jirani, yakiwemo Khojaly.

Mwaka 2020, baada ya mapigano ya siku 44, Azerbaijan ilikomboa miji, vijiji na makazi kadhaa katika eneo la Karabakh kutoka mikonono mwa Armeania waliozidhibiti kwa karibu miaka 30.

Azerbaijan ilirejesha mamlaka kamili katika Karabakh mwezi Septemba 2023 kufuatia operesheni iliyoitwa ya “kupambana na ugaidi,” baada ya vikosi vya wanaojitenga katika eneo hilo kujisalimisha.

Uturuki ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza kutambua matukio ya Khojaly kama mauaji ya halaiki, na imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kutaka haki itendeke kwa waathiriwa.

CHANZO:AA