| Swahili
Maoni
UTURUKI
5 dk kusoma
Austria na Uturuki: Hatua nyingine ya ushirikiano
Ziara ya Kansela Christian Stocker jijini Ankara inadhihirisha mwanzo mpya kati ya Austria na Uturuki. Katika kipindi ambacho kuna mizozo ya kisiasa, ushirikiano wa karibu siyo tu suala la msingi bali ni muhimu kimkakati.
Austria na Uturuki: Hatua nyingine ya ushirikiano
Rais wa Uturuki Erdogan akiwa na Kansela wa Austria Stocker jijini Ankara. (AA)

Na Muhammed Ali UCAR

Hatua ya Rais Recep Tayyip Erdogan kumlaki Kansela wa Austria Christian Stocker jijini Ankara kwa ziara yake rasmi ya kwanza nchini Uturuki ni ya muhimu zaidi kuliko ishara ya kidiplomasia. 

Ujumbe ulioelezwa katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari ulikuwa wazi: uhusiano umeimarika na umekuwa mzuri na sasa umeendelezwa katika maeneo mengine.

Hili pia ni muhimu. Bara Ulaya na maeneo mengine jirani yanakabiliwa na ukosefu wa usalama. 

Vita vya Ukraine, mapigano Mashariki ya Kati, mustakabali wa Syria, uhamiaji, nishati na usalama, na changamoto za kiuchumi zinafanya iwe vigumu kukabiliana na hali hizi peke yako. 

Kwa hiyo Austria na Uturuki wanatakiwa kuacha mazungumzo zaidi kuhusu yaliyowagawanywa katika siku za nyuma na badala yake wajadiliane kuhusu watakachofanikisha pamoja sasa hivi.

Uhusiano kati ya Austria na Uturuki ulitatizika kwa miaka kadhaa kutokana na taharuki ya kisiasa. Mijadala kuhusu uwezekano wa Uturuki kujiunga na EU na hasa shutuma za kisiasa ziliharibu uhusiano.

Kutokana na hayo, mjadala wa leo ni muhimu zaidi. Erdogan alieleza wazi kuhusu "muelekeo wenye tija" ambao ulifikiwa hivi karibuni katika uhusiano. 

Stocker, naye, alielezea Uturuki kama nchi muhimu na kupongeza jukumu la kidiplomasia la Uturuki katika vita vyote vya Ukraine na Mashariki ya Kati.

Hili linaonesha uhalisia wa kisiasa ambao nchi zote zinahitaji. Uhusiano mzuri haumaanishi kuwa Austria na Uturuki lazima wakubaliane katika kila jambo. 

Lakini, ni uhusiano wenye ishara kuwa kutofautiana hakuzuii majadiliano na ushirikiano.

Dola bilioni tano – na uwezekano wa kukuwa zaidi

Muelekeo huu mpya katika uhusiano wa kiuchumi unaonekana wazi. Biashara kati ya mataifa hayo mawili ilifika Dola bilioni 4.5 mwaka 2025. Lengo la mwaka huu ni Dola bilioni tano.

Kampuni zaidi ya 1,000 za Austria zinafanya kazi nchini Uturuki. Uwekezaji wa moja kwa moja kwa Austria sasa hivi umefika zaidi ya Dola bilioni kumi na moja, huku uwekezaji wa Uturuki nchini Austria ukifika karibu Dola bilioni moja. 

Hili linaonesha kuwa uhusiano wa kiuchumi kwa muda mrefu umekuwa zaidi ya njia za kawaida za biashara.

Pendekezo la Erdogan pia linaenda zaidi ya taasisi ziliopo na kuanzisha kamati ya pamoja ya kiuchumi na biashara kuchukua nafasi ya Tume ya Pamoja ya Uchumi, hilo ni la muhimu zaidi. 

Kama mkutano wake wa kwanza utafanyika kabla mwisho wa mwaka, ushirikiano wa sasa wa kisiasa utamaanisha kuwa ni mchakato wa kuwa na taasisi thabiti.

Hatua inayofuata inatakiwa iende zaidi ya uhusiano uliopo sasa wa biashara. Nishati safi, malighafi muhimu, teknolojia ya juu, uchukuzi, na sekta ya ulinzi inaonesha uwezekano mzuri. 

Ushirikiano kuhusu njia ya reli na Ushoroba wa Kati pia unaweza kuleta pamoja Austria na Uturuki kufanya kazi zaidi katika mitandao ya biashara kati ya Ulaya na Asia.

Hata hivyo, umuhimu wa uhusiano huu hauwezi kupimwa kwa takwimu za biashara pekee. Uturuki iko katikati ya yanayotokea katika changamoto za Ulaya.

Syria ni mfano muhimu zaidi wa hili. Erdogan aliweka wazi kuwa Uturuki iko tayari kushirikiana na Austria katika ujenzi mpya wa Syria

Syria yenye amani siyo kwa maslahi ya Uturuki pekee. Pia ni kwa maslahi ya Austria na Ulaya – kisiasa, kiuchumi, na zaidi kuhusu uhamiaji wa siku za baadaye.

Hilo pia ni kwa ajili ya Mashariki ya Kati. Kwa kuwa pande zote mbili zinasisitiza umuhimu wa diplomasia na ufikishwaji wa misaada kwa watu wa Gaza kama eneo la msingi la kuanza ushirikiano wao.

Zaidi ya hayo, kuna mataifa ya eneo la Balkan. Wote Uturuki na Austria wana uhusiano wa kihistoria, kiuchumi, na kijamii huko. Uthabiti wa mataifa ya Balkan, unaosisitizwa na mataifa yote mawili, kwa hiyo kwa ajili ya maslahi ya pamoja ya kimkakati.

Ushirikiano wa Austria na Uturuki pia unaweza kuwa na matokeo mazuri kwa uhusiano wa Uturuki na Umoja wa Ulaya.

Erdogan alizungumzia masuala mawili muhimu katika kikao chake na Stocker: kufanya umoja wa forodha kuwa wa kisasa na kuhusu uhuru wa viza. Masuala yote mawili hayatakiwi kuangaziwa kwa mtazamo wa utata wa kisiasa wa miaka iliopita.

Umoja wa forodha wa kisasa unaweza kuleta fursa kwa uchumi wa Ulaya na Uturuki hasa ikizingatiwa kuwa utaratibu wa usambazaji wa bidhaa na ushindani kimataifa. 

Maendeleo katika masuala ya viza yanaweza kusaidia katika ushirikiano wa biashara, sayansi na kijamii.

Austria haitakiwi kukubaliana na kila kitu ambacho Uturuki inapendekeza. Hata hivyo, inaweza kuchangia kwa kuhakikisha uhusiano kati ya Uturuki na EU unaangazia zaidi maslahi thabiti, majadiliano, na faida kwa wote. 

Uhusiano wa sasa kati ya Austria na Uturuki inaonesha inawezekana.

Jamii ya Waturuki ni sehemu ya ushirikiano huu

Suala moja ambalo halitakiwi kusahauliwa kwa watu wenye asili ya Uturuki nchini Austria. Tangu miaka ya 1960, vizazi kadhaa vimechangia zaidi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi hiyo.

Leo hii, watu wenye asili ya Uturuki ni wajasiriamali, wafanyakazi, madaktari, wanasayansi, wanafunzi, na wanamichezo. Wanatoa nafasi za ajira, wameanzisha biashara, na wakati huohuo kuchangia katika mshikamano wa watu mbalimbali nchini Austria.

Kwa hiyo jamii hiyo haitakiwi kuonekana tu kupitia suala la uhamiaji na ujumuishaji.

Wakati uhusiano wa kisiasa unapoimarika, masuala haya ya kijamii pia yanafaidika. Watu Wanaojua mataifa yote mawili, lugha, na tamaduni wanakuwa na jukumu muhimu la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii.

Ziara ya Stocker inadhihirisha muelekeo kati ya Uturuki na Austria ulivyobadilika. Miaka michache iliopita, uhusiano ulikuwa wa utata. Leo hii, wanaangazia biashara, uwekezaji, usalama, uhamiaji, diplomasia, uchukuzi, nishati, na usalama katika kanda.

Hii ni hatua ambayo nchi zote zinatakiwa kuikumbatia.

Austria iko katikati mwa Ulaya, Uturuki iko kusini mashariki kimkakati na karibu na Bahari Nyeusi, eneo la Caucasus na Mashariki ya Kati. Kwa sababu hii mahsusi, masuala yenye tija hayatakiwi kuishia kwenye ziara moja moja pekee. 

Mawasiliano ya mara kwa mara kisiasa, mifumo mipya ya kiuchumi, ushirikiano zaidi wa kijamii, na majadiliano yenye tija kati ya Uturuki na EU yanaweza kubadilisha hili na kuwa ushirikiano wa muda mrefu.

Uhusiano wa zamani kati ya Austria na Uturuki haukuwa mzuri. Lakini kutokana na changamoto za sasa, itakuwa makosa kuruhusu itoe muelekeo wa mustakabali. Ziara ya Stocker nchini Uturuki ni ishara nzuri kuwa pande zote zinatambua hili.

(Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza katika TRT Deutsch)

CHANZO:TRT World
Soma zaidi
Putin: Uturuki ni mshirika wa kweli wa kiuchumi na wa kidiplomasia
Erdogan, Putin wapongeza ushirikiano wa Uturuki na Urusi katika mkutano wa SCO
Uturuki kuongeza ushirikiano na Muungano wa Ushirikiano wa Shanghai: Rais Erdogan
Mkataba wa Ulinzi wa Makkah waweka msingi wa kujenga mfumo mpya wa usalama wa kikanda: Fidan
Uturuki, Pakistan na Saudi Arabia kufanya mkutano wa kwanza wa makubaliano ya ulinzi ya Makka
Operesheni ya uokoaji inaendelea baada ya kivuko kupinduka karibu na TRNC
Agosti 30: Ushindi uliofungua njia ya kuinuka kwa Uturuki ya kisasa
Erdogan ameisifu Uturuki katika maadhimisho ya miaka 104 ya 'Siku ya Ushindi'
Jeshi la Wanamaji la Uturuki na vikosi vya Somalia vyaokoa meli ya mizigo iliyotekwa na maharamia
Uturuki yataka kupunguza mizozo katika Ulimwengu wa Kiislamu: Erdogan
Rais Erdogan ajadili amani ya kikanda na viongozi wa Rwanda na DRC
Erdogan: Uturuki itaendelea kufanya maendeleo licha ya migogoro ya kikanda
Erdogan na Lula wajadili kuimarisha zaidi uhusiano wa kiuchumi
Katika picha: Waogeleaji 2,500 wavuka Mlango-bahari wa Istanbul katika mbio za kila mwaka za mabara
Uturuki yataka ilani nyekundu ya Interpol dhidi ya Netanyahu kufuatia shambulio dhidi ya fotilla
Uturuki kuimarisha uwezo wa jeshi lake la wanamaji: Waziri wa Ulinzi
Waziri wa zamani wa ulinzi wa Israel Yaalon amshtumu Netanyahu kwa uchokozi dhidi ya Uturuki
Uturuki itaendelea kuwa chanzo cha matumaini kwa Gaza na dunia: Erdogan
Kenya, Uturuki kushirikiana zaidi katika biashara, uwekezaji na ulinzi
Uturuki yachapisha rasmi sheria ya mchakato wa 'Uturuki Isiyo na Ugaidi'