CAF kufanya mabadiliko ya kanuni baada ya fainali za Afcon

Tangazo hilo lilifuatia kikao cha kamati kuu ya CAF mjini Cairo siku ya Jumapili na linakuja siku ya tafrani kwa shirika hilo baada ya katibu mkuu wake akijiuzulu.

By
Patrice Motsepe, Rais wa Shirikisho la soka CAF / Reuters

Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF limesema litatekeleza mabadiliko na uboreshaji wa sheria na kanuni zake ambazo zitahakikisha kwamba matukio tete kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya Januari hayatafanyika tena.

Rais wa CAF Patrice Motsepe alisema mabadiliko hayo yataimarisha imani kwa waamuzi wake, waendeshaji wa VAR na vyombo vya mahakama lakini hakutoa maelezo kamili.

Tangazo hilo lilifuatia kikao cha kamati kuu ya CAF mjini Cairo siku ya Jumapili na linakuja siku ya tafrani kwa shirika hilo baada ya katibu mkuu wake akijiuzulu.

Shirikisho la soka barani Afrika limekuwa likipambana na tatizo la kutoaminika baada ya Bodi yake ya Rufaa kuipokonya Senegal taji la Kombe la Mataifa ya Afrika katika uamuzi ambao umekabiliwa na kejeli nyingi.

Pingamizi mahakamani

Senegal iliamuliwa kuwa wamepoteza mchezo wa fainali mjini Rabat Januari 18 baada ya kutoka nje ya uwanja wakipinga mkwaju wa penalti ambao ulitolewa kwa Morocco.

Walirejea na kufunga bao katika muda wa nyongeza na kushinda 1-0.

Uamuzi huo unapingwa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo na ikiwa Senegal itashinda tena taji lao itakuwa pigo zaidi kwa uaminifu wa CAF.

"CAF imechukua ushauri wa kina wa kisheria kutoka kwa wanasheria na wataalam wakuu wa soka barani Afrika na kimataifa, ili kuhakikisha kuwa sheria na kanuni za CAF zinazingatia na kutekeleza kanuni bora za soka duniani, ndani na nje ya uwanja," Motsepe alisema katika taarifa yake Jumapili.

Heshima na Uadilifu wa CAF

"Hii ni muhimu kwa heshima, uadilifu na uaminifu wa waamuzi wa Kiafrika, waendeshaji wa VAR na Bodi ya Nidhamu ya CAF na Bodi ya Rufaa.

"CAF inashirikiana na FIFA kwa mafunzo yanayoendelea ya waamuzi wa Kiafrika, waendeshaji wa VAR na makamishna wa mechi ili wawe bora kama wachezaji bora zaidi duniani kote.

CAF imepata maendeleo makubwa katika miaka mitano iliyopita katika kutekeleza utawala, maadili, uwazi na usimamizi bora," rais wa CAF aliongeza.

Maelezo sahihi zaidi kuhusu mabadiliko na jinsi wangeepuka kurudiwa kwa mzozo wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika hayakutolewa na Motsepe, ambaye mapema mwezi huu alikiri shirika lake lilikuwa likipambana na mitazamo kuhusu uadilifu wake.