Meli ya Uturuki ya kuchimba mafuta baharini yawasili Somalia kwa operesheni ya kwanza nje ya nchi
Waziri wa Nishati wa Uturuki Alparslan Bayraktar amepongeza "ukurasa mpya" katika ushirikiano wa nishati kati ya Uturuki na Somalia baada ya meli ya kuchimba mafuta ya Çağrı Bey kuwasili Somalia.
Meli ya Uturuki ya uchimbaji mafuta baharini imewasili nchini Somalia kwa “shughuli ya kihistoria,” ishara ya kuanza kwa operesheni ya kwanza ya kuchimba mafuta baharini nje ya nchi kwa Uturuki, waziri wa nishati na maliasili wa Uturuki alitangaza siku ya Alhamisi.
“Çağrı Bey (meli) imewasili Somalia kwa operesheni ya kihistoria,” Alparslan Bayraktar alisema kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki NSosyal, akiongeza kuwa operesheni hiyo itafungua “ukurasa mpya katika historia ya nishati ya nchi zote mbili za Uturuki na Somalia.”
Anasema Uturuki inaanza uchimbaji mafuta wake wa kwanza baharini nje ya nchi, akiongeza: “Tunaomba rehema za Mungu kwa operesheni yetu ya kwanza ya mafuta baharini nje ya mipaka yetu.”
Kulingana na Wizara ya Nishati ya Uturuki, Çağrı Bey inatarajiwa kuchimba kisima cha Curad-1 na kwenda kina cha mita 7,500 (zaidi ya futi 24,600) kwa zaidi ya muda wa siku 288.
Bayraktar alisema mapema mwezi huu kuwa meli hiyo ingewasili Somalia siku ya Ijumaa na kuwasili kwake, Uturuki itaanza uchimbaji wake wa kwanza katika bahari ya taifa hilo la Pembe ya Afrika.