| Swahili
MICHEZO
3 dk kusoma
Rais Erdogan awapongeza "Masultani wa Wavu" kufuatia ushindi wa Ligi ya Mataifa
Uturuki imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mataifa ya Mpira wa Wavu kwa mara ya pili, baada ya kufuzu kushiriki hatua ya fainali kwa mwaka wa nane mfululizo.
Rais Erdogan awapongeza "Masultani wa Wavu" kufuatia ushindi wa Ligi ya Mataifa
Uturuki yatwaa ubingwa wa la Ligi ya Mataifa ya Wanawake kwa ushindi dhidi ya Brazil. / / AA

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameipongeza timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa wavu baada ya kuifunga Brazil katika fainali ya Ligi ya Mataifa ya mwaka 2026 na kutwaa ubingwa.

"Nawapongeza kwa moyo wangu wote timu yetu ya taifa ya wanawake ya mpira wa wavu, ambayo imeifanya Uturuki kujivunia kwa kupata mafanikio makubwa kwa kuifunga Brazil katika fainali ya Ligi ya Mataifa na kuwa mabingwa," Rais Erdoğan alisema kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye akaunti yake ya NSosyal siku ya Jumapili.

Katika mazungumzo ya simu yaliyofanyika kando, kiongozi huyo wa Uturuki aliwapongeza wote waliochangia mafanikio ya timu ya taifa, hususan wachezaji na benchi la ufundi.

Timu ya taifa ya wanawake ya Uturuki imeifunga Brazil kwa seti 3-1 katika fainali hiyo na kutwaa ubingwa huo kwa mara ya pili katika historia yake.

Mechi ya fainali ilifanyika katika ukumbi wa East Asian Games Dome uliopo Macau, China, ambapo Uturuki ilikabiliana na Brazil, timu iliyokuwa ikishika nafasi ya pili duniani.

Kwa ushindi wa seti 3-1 dhidi ya Brazil, Uturuki iliongeza ubingwa wa pili wa Ligi ya Mataifa ya Mpira wa Wavu baada ya kutwaa taji lake la kwanza mwaka 2023.

Uturuki imeshinda ubingwa huo kwa mara ya pili baada ya kufuzu hatua ya fainali kwa miaka minane mfululizo tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 2018.

Timu hiyo maarufu "Masultani wa Wavu" (Sultans of the Net) ilionyesha kiwango cha juu kwa kuifunga China katika hatua ya nusu fainali na kufuzu kushiriki mchezo wa kuwania ubingwa.

Timu ya taifa ilitwaa taji lake la kwanza kwa kuifunga China katika fainali ya mwaka 2023, baada ya kumaliza katika nafasi ya pili katika fainali ya mwaka 2018 dhidi ya Marekani.

Baada ya kurejea tena fainali miaka mitatu baadaye, Uturuki imeongeza jumla ya medali zake katika mashindano kuwa nne: medali mbili za dhahabu, moja ya fedha na moja ya shaba, na hivyo kuwa miongoni mwa timu zilizofanikiwa zaidi katika historia ya mashindano hayo.

Kocha mkuu wa timu ya taifa, Daniele Santarelli, ameendelea kuandika historia ya mafanikio akiwa na Uturuki.

Kocha huyo raia wa Italia, aliyeteuliwa kuinoa timu mwaka 2023, ametwaa medali yake ya tatu ya dhahabu akiwa na timu ya taifa.

Baada ya kuiwezesha Uturuki kushinda ubingwa wa Ligi ya Mataifa mwaka 2023, Santarelli ameiongoza tena timu hiyo kutwaa taji hilo mwaka 2026. Pia aliiongoza Uturuki kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2023.

Santarelli pia aliiongoza Uturuki kushinda medali ya fedha katika Mashindano ya Dunia ya Wanawake ya FIVB mwaka 2025, na kufikisha jumla ya medali zake akiwa na timu ya taifa kuwa nne.

Ushindi huo pia uliiwezesha Uturuki kulipiza kisasi kwa Brazil kufuatia kipigo ilichopata katika mchezo wa kuwania medali ya shaba kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.

Miaka miwili baada ya kupoteza dhidi ya Brazil mjini Paris, Uturuki ilikutana tena na mpinzani huyo katika mchezo mwingine wa kuwania medali na safari hii ikaibuka mshindi kwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mataifa ya Mpira wa Wavu.

Brazil ilikuwa imepoteza fainali za Ligi ya Mataifa dhidi ya Marekani mwaka 2018, 2019 na 2021, kabla ya kufungwa na Italia katika fainali ya mwaka 2025, na hatimaye kupoteza tena mbele ya Uturuki katika fainali ya mwaka 2026.

CHANZO:AA
Soma zaidi
FIFA yakanusha madai ya Morocco ya 'uwenyeji' wa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2030
Erdogan akutana na timu ya Voliboli ya wanawake ya Uturuki baada ya ubingwa wa Ulaya
Timu ya wasichana ya Tanzania ya chini ya umri wa miaka 15 imetwaa ubingwa wa CECAFA
Mshambuliaji Aubameyang astaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Gabon
Antonio Rüdiger astaafu kuichezea timu yake ya taifa
Jepchirchir anaongoza ushindi wa 1-2 kwa Kenya jijini Sydney
Gobena avunja rekodi ya Sydney Marathon huku Ethiopia ikitawala mbio za wanaume
Fenerbahce yaifunga Lyon 2-1 kuiwezesha kurejea Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya misimu 17
Mkuu wa Shirikisho la UEFA hataki nafasi ya Infantino, anachotaka ni ajiuzulu
Bondia wa zamani bingwa wa dunia Zolani Tete auawa kwa kupigwa risasi nchini Afrika Kusini
Guinea yatangaza nia ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika
FIFA yawaadhibu wachezaji wa Argentina, yaitoza faini shirikisho kwa matukio ya Kombe la Dunia
Cristiano Ronaldo atangaza azma yake ya kustaafu soka
Algeria imefanikiwa kupata medali kwa mara ya kwanza katika mashindano ya WAFCON baada ya kuishinda
Afrika Magharibi ving’ang'anizi kwa mara ya kwanza kwa nafasi ya tatu WAFCON
Madada wawili wa Malawi kuendelea kuibeba timu fainali za WAFCON dhidi ya Cameroon
PSG kuikabili Aston Villa fainali ya UEFA Super Cup nchini Austria
Nairobi yawasilisha ombi la kuandaa Mashindano ya Dunia ya Riadha 2029
Trump aionya FIFA kuhusu kumtimua Gianni Infantino
Josephine Sembeyo wa Kenya ashinda dhahabu ya mita 1500 katika Mashindano ya Dunia ya Vijana (U20)