Kamanda wa jeshi la Sudan atoa wito wa kuhamasisha umma dhidi ya RSF

Kamanda mwandamizi wa jeshi la Sudan ametoa wito kwa raia kuitikia ombi la kiongozi wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan wa kutaka waungane nchini nzima dhidi ya wapiganaji wa RSF.

By
Watu wasiopungua 40,000 wameuawa Sudan tangu vita vilipoanza Aprili 2023. / Picha: AP

Kamanda mwandamizi wa jeshi la Sudan amewataka raia kuitikia wito wa Mkuu wa Majeshi Abdel Fattah al-Burhan kuungana na wenzao nchi nzima dhidi ya wapiganaji wa RSF.
Ali Hassan Bello, kamanda wa eneo la Kiulinzi la Blue Nile, aliwapongeza wanajeshi, vikosi washirika, na umma “kwa ushindi waliopata enep la Kordofan dhidi ya wapiganaji.”
“Ushidni tutaupata katika miji iliyobaki,” alisema katika taarifa iliyosomwa na shirika la habari la serikali SUNA.


Aliwaomba vijana wa Sudan kuitikia wito wa Mkuu wa Majeshi wa kutaka wajitolee dhidi ya wapiganji hao.

Wito wa nchi nzima
Siku ya Jumamosi, Burhan, ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Sudan, alitoa wito kwa nchi nzima dhidi ya wapiganaji wa RSF.
Siku ya Jumanne, jeshi lilisema kuwa limepata mafanikio makubwa katika maeneo kadhaa Kordofan baada ya makabiliano na RSF.
Jeshi limesema “maeneo muhimu” yako salama, na kuapa kuendelea na mapigano dhidi ya RSF “hadi nchi itakapokuwa haina uasi na ajenda ya mataifa ya kigeni.”
Wakati huohuo, Jeshi la Sudan limedungua ndege isiyokuwa na rubani siku ya Jumatano katika eneo la Al Obeid, mji mkuu wa Jimbo la Kordofan Kaskazini, walioshuhudia walisema.

Ushindi mkubwa kwa jeshi
Wanaharakati wa Sudan wameweka video katika mitandao ya kijamii zikionesha mitambo yao ya ulinzi yakidungua ndege zisizo na rubani kabla kuanguka.
Hakukuwa na taarifa yoyote kutoka kwa RSF kuhusu tukio hilo.

Siku ya Jumanne, muungano wa vikosi vinavyounga mkono jeshi, ulisema wamechukuwa udhibiti wa Abu Sunun na Abu Qaoud jimbo la Kordofan Kaskazini.
Siku moja kabla ya hapo, jeshi la Sudan lilisema limechukuwa tena eneo la Um Sayala huko Kordofan Kaskazini kutoka kwa RSF.