| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania: Rais Samia atangaza mpango wa kubana matumizi
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dodoma, mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.
Tanzania: Rais Samia atangaza mpango wa kubana matumizi
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. / Ikulu Tanzania
tokea masaa 11

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, amesema kuwa, ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa mafuta pamoja na kupunguza matumizi ya serikali, ofisi yake imeanza kuchukua hatua za kubana matumizi, ikiwemo kupunguza ukubwa wa msafara.

Kulingana na Rais Samia, maofisa watakaokuwa katika msafara wake watatumia gari moja badala ya magari mengi, hatua inayolenga kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

Hata hivyo, Rais Samia amesisitiza kuwa kupanda kwa bei ya mafuta si tatizo linalosababishwa na Tanzania pekee, bali ni changamoto ya kimataifa.

Aidha, amezitaka taasisi zote zilizo chini ya mamlaka yake kuhakikisha zinachukua hatua madhubuti za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kuimarisha matumizi bora ya rasilimali za umma.

Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dodoma, mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.

CHANZO:TRT Afrika Swahili