| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
UNICEF inasema watoto wasiopungua 20 wameuawa mwezi Januari nchini Sudan
Shirika hilo linaonya kuwa mamilioni ya watu wanahitaji msaada huku njaa kali ikienea maeneo mengine yanayokabiliwa na mapigano
UNICEF inasema watoto wasiopungua 20 wameuawa mwezi Januari nchini Sudan
Sudan./ AA
tokea masaa 14

Watoto wasiopungua 20 wameuawa mwezi Januari nchini Sudan, wengi wao katika maeneo ya Kordofan na Darfur magharibi mwa Sudan, UNICEF ilisema siku ya Ijumaa.

Vifo hivyo vimeorodheshwa kwenye ripoti iliyoandikwa na shirika hilo la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto likiangazia watoto katika kanda nzima, ikiwemo Sudan.

“Nchini Sudan, mwenzi Januari 2026, watoto wasiopungua 20 wameuawa, wengi wao katika majimbo ya Kordofan na Darfur,” UNICEF ilisema.

Shirika hilo limeonya kuwa “mamilioni ya watoto nchini Sudan wanahitaji misaada, ulinzi na kurudishwa kwa huduma muhimu” huku mapigano yakiendelea katika maeneo mengi nchini humo.

UNICEF inasema njaa kali tayari imethibitishwa huko Al Fasher Kaskazini mwa Darfur na Kadugli huko Kordofan, huku maeneo mengine 20 yakiwa katika hatari.