| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Trump: Marekani inapigana na Iran kulinda washirika wake
Trump pia amedai kuwa Iran inaweza kuwa tishio kwa Ulaya na baadhi ya miji ya Marekani katika siku zijazo.
Trump: Marekani inapigana na Iran kulinda washirika wake
Rais Trump amesema Marekani “inafanya vizuri sana” katika kukabiliana na Iran. /

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa Marekani inaikabili Iran kwa lengo la kulinda washirika wake wa Mashariki ya Kati pamoja na mataifa ya Magharibi dhidi ya mashambulizi yanayoweza kutokea.

“Tunafanya hivyo kusaidia Mashariki ya Kati. Tunafanya hivyo kusaidia Israel. Na tunafanya hivyo kujilinda wenyewe, kwa sababu baada ya kuiangamiza Israel, jambo ambalo wangelifanya kwa furaha kubwa, na kisha kuishambulia Mashariki ya Kati, wangekuja kuishambulia Ulaya na baadhi ya miji yetu,” alisema Trump Jumatano.

Wakati huo huo, amesema kuwa Marekani “inafanya vizuri sana” katika kukabiliana na Iran. 

Kauli hizo zilitolewa wakati mapigano kati ya Marekani na Iran yalipozuka tena baada ya kipindi cha takribani mwezi mmoja cha utulivu.

Mwishoni mwa wiki, Marekani ilishambulia vitua vya kurusha roketi vilivyokuwa kwenye Kisiwa cha Larak, nchini Iran. Iran ilijibu kwa kurusha makombora kuelekea Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Siku ya Alhamisi, ving’ora vya tahadhari vilisikika nchini Kuwait, huku mifumo ya ulinzi wa anga ikijaribu kuzuia mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani.

Wizara ya Ulinzi ya Kuwait ilieleza kwenye mtandao wa X kuwa ilikuwa inakabiliana na kile ilichokiita “uchokozi wa wazi wa Iran.”

Mapigano yamezidi kushika kasi tangu jeshi la Marekani liliposhambulia maeneo ya Iran yaliyoko kwenye kisiwa katika Mlango-Bahari wa Hormuz mwishoni mwa wiki. Marekani ilisema ilifanya shambulio hilo kwa sababu Iran ilikuwa inapanga kutumia maeneo hayo kuweka mabomu ya ardhini, baharini.

Iran ilijibu kwa kurusha makombora kuelekea vituo vya kijeshi vya Marekani nchini Jordan, lakini makombora hayo yalinaswa na mifumo ya ulinzi wa anga.

CHANZO:TRT World and Agencies
Soma zaidi
Nepal yaruhusu kilimo cha bangi
Panya buku mwenye kilogramu 30 agundulika Thailand
Kiongozi wa upinzani nchini Israel aondoa uwezekano wa kuunda serikali ya umoja na Netanyahu
Trump: Vita dhidi ya Iran vilichangia kushindwa kwa chama cha Republican katika uchaguzi
Wapiganaji wa Iran wadai kushambulia droni mbili za Marekani kwenye Mlango Bahari wa Hormuz
Ajali ya helikopta juu ya Mlima Everest yaua mtalii wa kihindi
Putin asema Urusi ni mshirika bora kwa Afrika kuliko nchi zenye historia ya ukoloni
Netanyahu aongoza, hatima ya kuunda serikali bado haijulikani
Rais Lula wa Brazil atimiza miaka 81, aahidi kufanya kazi saa 24
Lieberman ataka Netanyahu achunguzwe kwa tuhuma za uhaini kuhusiana na vita dhidi ya Iran
Rais wa Brazil Lula da Silva apata ushindi wa kihistoria wa muhula wa 4 dhidi ya Flavio Bolsonaro
Maandamano Ufaransa yakigeuka kuwa ya vurugu, huku maelfu wakikamatwa katika miji tofauti
Maelfu ya Waisraeli waandamana Tel Aviv kudai kukomeshwa kwa enzi ya Netanyahu kabla uchaguzi
Papa Leo XIV ahairisha ziara ya Assisi kwa ushauri wa madaktari
Marekani yawaagiza wanadiplomasia wake na familia zao kuondoka nchi za Ghuba
Trump asema Marekani haijadiliani na Iran, aashiria kuwashughulikia 'hivi karibuni'
Iran kuzindua bomu lake kubwa zaidi “father of all bombs”
Uturuki, Qatar, Indonesia na Pakistan zasaini makubaliano ya ushirikiano wa ulinzi ya 'Badr'
Uingereza kupeleka ndege za kivita Saudi Arabia kuilinda dhidi ya mashambulizi ya Wahouthi
Makamu wa Rais wa Ufilipino, Sara Duterte apinga kung’olewa madarakani