| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Waafrika waliokuwa India kwa matibabu, miongoni mwa 21 waliofariki katika ajali ya moto hotelini
Waziri Mkuu Narendra Modi amesema ajali hiyo "ni mbaya" huku operesheni ya uokoaji ikiendelea.
Waafrika waliokuwa India kwa matibabu, miongoni mwa 21 waliofariki katika ajali ya moto hotelini
Wazima moto wakiwa katika hoteli mjini New Delhi, India, tarehe 3 Juni 2026. / AP

Takriban watu 21 wamefariki katika ajali ya moto iliyotokea katika hoteli huko New Delhi Jumatano. Polisi imesema kuwa jali hiyo ni mbaya zaidi kutokea katika mji mkuu wa India katika miaka ya hivi karibuni.

Baadhi ya waliofariki ni raia wa Afrika ambao walifika kwa ajili ya matibabu, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Ajali za moto hutokea mara kwa mara katika majengo nchini India kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuzimia moto na kutozingatia kanuni za usalama.

Moto umewaka katika hoteli ya Flourish Stay, katika eneo la makazi ya watu wengi kusini mwa mji huo, kwa mujibu wa polisi wa Delhi.

"Inasikitisha sana kwamba watu 21 wamefariki katika ajali hii mbaya," polisi imesema.

Uokoaji na utafutaji

Polisi imesema, zoezi la uokoaji na utafutaji linaendelea, huku zaidi ya watu 40 wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Moto huo hatimae ulizimwa kwa msaada wa gari nane za kuzimia moto, polisi imesema.

"Wahusika wote wamepelekwa katika eneo la tukio kuhakikisha msaada kamili unawafikia walioathirika," polisi imeongeza kusema.

Waziri Mkuu Narendra Modi ameliita tukio hilo "baya zaidi."

"Salam zangu za rambirambi kwa waliopoteza wapendwa wao," imesema ofisi yake kupitia mtandao wa X.

Chanzo hakijajulikana

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

Hitilafu za umeme, bado ni chanzo kikubwa cha ajali za moto India.

Mwezi Machi, moto uliotokea katika hospitali ya serikali mashariki mwa India uliuwa takriban wagonjwa 10 waliokuwa mahututi.

Soma zaidi
Iran yatishia kushambulia mitambo ya umeme ya nchi za Ghuba iwapo Marekani itashambulia mitambo yake
Nchi 20 za Kiislamu zajadili hatua za pamoja dhidi ya ukiukaji wa Israel katika Msikiti wa Al-Aqsa
Mawaziri wa bara Arabu, Waislamu wakutana Jordan kujadili kwa pamoja Jerusalem Mashariki inayokaliwa
Wahamiaji 70,000 waondoka Hispania huku idadi ya vifo ikiongezeka
Wanafunzi wa Korea Kusini matatani kwa ‘kuvunja’ na kuingia ndani ya kambi ya kijeshi ya Marekani
Wahamiaji wapatao 160 waokolewa baada ya meli yao kuwaka moto
Chama cha soka cha Palestina chaituhumu FIFA kwa kushindwa kuiadhibu Israel
Trump aitaka Iran ichague kati ya makubaliano na kujislamisha
Namna kijana mwenye umri wa miaka 12 mwenye usonji alivyotumia uokaji keki kukabiliana na chuki
Australia yathibitisha vifo vya ndege vinavyotokana na mafua H5
Iran: Hatuna mazungumzo yoyote na Marekani
Mashambulizi ya Israel yaua Wapalestina 12, wakiwemo watoto wawili, huko Gaza
Iran inachukulia kila tishio kutoka kwa wapinzani kuwa "halisi na la kuaminika" : Kaimu Waziri
Trump asitisha shambulio lililopangwa dhidi ya Iran
Hamas yakubali kusalimisha silaha nzito katika 'uamuzi mgumu' kama sehemu ya makubaliano
Makubaliano ya nyuklia ya Marekani na Saudi Arabia yanabadilisha muelekeo Mashariki ya Kati
Taifa la Nauru labadilisha jina, sasa kuitwa Naoero
China yakana taarifa za kusafirisha vifaa vya kurusha makombora Iran
Marekani yaanzisha wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Iran
Watu wasiojulikana waharibu kituo cha hija ya Wakatoliki nchini Bosnia