Komesha vita vya Marekani- Israel dhidi ya Iran kabla ya kulikumba eneo lote, aonya rais Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasisitiza kuwa suluhisho la kidiplomasia 'linawezekana kabisa,' akiangazia mtazamo wa tahadhari wa Uturuki huku kukiwa na mvutano wa kikanda.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa wito wa kusitishwa kwa vita vinavyoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran kabla havijaongezeka na kulikumba eneo hilo, akisisitiza kuwa suluhu la kidiplomasia bado "linawezekana kabisa" iwapo litapewa nafasi.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kundi la wabunge wa chama chake siku ya Jumatano, Erdogan alisema Uturuki "inaendeleza kwa subira juhudi za kurejea kwenye meza ya mazungumzo na kufufua diplomasia."
Ameongeza kuwa, kutokana na unyeti wa hali hiyo, Uturuki anazungumza kwa tahadhari na kuchukua hatua makini ili kujilinda na migogoro inayoizunguka.
Rais pia alisisitiza kuwa Uturuki haifungii jicho mizozo katika eneo hilo na haiwapi kisogo marafiki na ndugu wakati wa shida.