| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Waethiopia washinda kesi dhidi ya Trump kuhusu kutimuliwa Marekani
Jaji mmoja nchini Marekani amezuia hatua ya kumaliza hadhi ya kinga kwa zaidi ya raia 5,000 wa Ethiopia, inayofahamika kama Hadhi ya Kinga ya Muda (TPS).
Waethiopia washinda kesi dhidi ya Trump kuhusu kutimuliwa Marekani
Serikali ya rais Donald Trump imekuwa ikiwasaka na kuwaondoa wahamiaji chini ya agenda ya "Marekani Kwanza". / Reuters
tokea masaa 7

Rais wa Ethiopia wameshinda kesi muhimu dhidi ya serikali ya Donald Trump kwa jaribio lake la kutaka kuwatimua nchini Marekani.

Jaji mmoja nchini Marekani amezuia hatua ya kumaliza hadhi ya kinga kwa zaidi ya raia 5,000 wa Ethiopia, inayofahamika kama Hadhi ya Kinga ya Muda (TPS).

Mpango huo, ambao ulianzishwa 1990, unaruhusu wahamiaji kuishi na kufanya kazi Marekani huku wakiwa na kinga ya kutoondolewa nchini humo.

Unakuwepo kwa watu ambao nchi zao zimekumbwa na majanga ya asili, mapigano au matukio mengine ambayo yanawaweka hatarini.

Kwa miaka mingi, maelfu ya wahamiaji, wengi kutoka bara la Afrika, Asia, Marekani ya Kusini na Karibe, wamefaidika na mpango huo.

Msako wa wahamiaji

Hata hivyo, serikali ya Trump, ambayo inaendelea na msako wa wahamiaji chini ya agenda yake ya "Marekani Kwanza", imetaka kuondoa sera hiyo ya muda mrefu kwa raia wa mataifa yasiyopungua 13, ikiwemo Somalia, Sudan, Cameroon na Sudan Kusini.

Uamuzi huu uliowapa ushindi raia wa Ethiopians wa Jaji Brian Murphy huko Boston ni pigo kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani.

Mapigano nchini Ethiopia

Hata hivyo, serikali ya Trump ilitangaza Disemba mwaka uliopita kuondoa mpango wa TPS kwa raia wa Ethiopia, ikisema kuwa hali nchini mwao imeimarika na ni salama kwao kurudi.

Imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kuwa TPS "haikutakiwa kuwa fursa ya kupata makazi ya kudumu".

Baadhi ya raia wa Somalia pia waliwasilisha kesi kama hiyo mwezi Machi, ikipinga mipango ya kuwaondolea haki za TPS.

CHANZO:TRT Afrika and agencies