Afrika ijiandaee na mashambulizi ya muda mrefu ya Marekani-Israel dhidi ya Iran
Hadi kufikia sasa, gharama za mafuta duniani zimepanda kwa asilimia 10.
Licha ya kupita juu ya anga za Mashariki, bado athari zake zinaonekana wazi ndani ya bara la Afrika.
Dunia imekuwa kwenye taharuki kubwa, toka siku ile Marekani na Israel, zilipofanya mashambulizi ya pamoja dhidi ya Iran.
Bara la Afrika halipaswi kubaki kama mtazamaji tu wakati haya yote yakiendelea. Ni lazima lijiandae kwa uwezekano wa kuendelea kwa vita hivi na madhara yake kwa bara hilo.
Kwa sasa, kumekuwepo na mitazamo tofauti kuhusu yanayoendelea ulimwenguni kwa sasa.
Katika pembe ya Afrika, serikali zimeendelea kuikosoa Iran, huku zikiwa kimya kwa yale yanayofanywa na Marekani na Israel.
Somaliland, ambayo bado inasubiri kutambuliwa rasmi, imekuwa upande wa Israel.
Waziri Mkuu wa Ethiopia alimpigia simu mwana mfalme wa Kuwait, kuilaani mashambulizi hayo.
Hata hivyo, hali ya tahadhari bado inaendelea kuchukuliwa katika upande wa Afrika Magharibi, huku Nigeria, Ghana na Senegal zikishindwa kulaani moja kwa moja.
Kwa upande wake, Afrika Kusini imechukua mwelekeo tofauti kabisa, kwa kurejelea sheria za kimataifa hususani kwenye suala la ulinzi binafsi.
Kama tu Waziri Mkuu wa Senegal alivyoonya, "taifa lolote lile, bila idhini kutoka Umoja wa Mataifa, linaweza kushambulia nchi nyingine na kuua viongozi wa nchi hiyo. Hili ni suala linalopaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi ".
Mipasuko hii ya kidiplomasia inaonesha hali ilivyo mbaya. Bara la Afrika halipaswi kubaki kuwa kama mtazamaji tu katika mgogoro huo.
Athari za kiuchumi Afrika
Kwa sasa, Mlango wa Hormuz, ambao hupitisha asilimia zipatazo 30 za meli za mafuta na gesi, umekuwa eneo la vita.
Iran imevitaka vyombo hivyo kukwepa njia hiyo, huku taasisi ya kifedha ulimwenguni ya JPMorgan, ikionya kuwa, pipa moja la mafuta litauzwa kwa zaidi ya dola 100, iwapo vita hivyo vitaongezeka.
Hili si suala la kusadikika kwa bara la Afrika, kwani litaathiri bajeti za kaya na zile za kitaifa.
Wazalishaji mafuta mbalimbali duniani kama vile Nigeria, Angola na Gabon, zinaweza kufaidika na faida za mapato.
Kwa upande mwingine, Nigeria na Angola zimeondoa ruzuku kwenye mafuta, hatua inayowaweka watumiaji njia panda.
Kwa waigizaji wa mafuta kama vile Kenya, Zambia, Rwanda, Afrika Kusini na Ghana, hali inaonekana mbaya zaidi.
Kupanda kwa gharama za mafuta, kutasababisha kupanda kwa gharama zingine za bidhaa muhimu.
Ikumbukwe kuwa, bado mataifa mengi yanazinduka kutoka mlipuko wa UVIKO-19 na mzigo mwengine wa madeni.
Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imeonya kuwa, njia muhimu zenye kuunganisha Mlango wa Hormuz, zinawezesha usafirishaji wa bidhaa za nishati na nyinginezo kati ya Asia, Ulaya na Afrika.
Hata hivyo, utaratibu mzima unaweza kuvurugika, iwapo kutaibuka tatizo la aina yoyote ile, kama vile wakati wa UVIKO-19 na vita kati ya Urusi na Ukraine.
Tishio la usalama kwenye kanda yetu
Mgogoro unaoendelea unaweza kuwa na athari kubwa barani Afrika.
Hadi kufikia sasa, idadi kubwa ya wafuasi wa Kishia, wameanza kuingia mitaani.
Kwa mfano, nchini Nigeria, Vuguvugu la Kiislamu nchini humo (IMN), limeandaa maandamano katika miji iliyoko kaskazini mwa nchi hiyo, huku waandamanaji wakibeba bendera za Iran na kutoa kauli za kuilaani Israel.
Polisi nchini humo, wameweka msisitizo kwenye uchunguzi na ufuatiliaji, wakionya kwamba, nchi hiyo haitokuwa jukwaa la migogoro ya nje.
Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanaonya kuwa, Afrika inaweza kufuatia katika migogoro ya aina hii.
Nguzo tano za ustahimilivu kwa bara la Afrika
Ni vyema, kuongeza kasi ya mifumo barani mwetu, ili tujikinge na migogoro ya kifedha ulimwenguni.
Mgogoro huu unatufundisha hasara za kutegemea fedha za nje katika kufanya biashara zetu wenyewe kama Waafrika.
Jambo la pili ni kuwa, ni lazima kutumia rasilimali zetu vizuri kwa faida ya bara zima.
Asilimia 30 ya madini adimu duniani, yanatokea Afrika.
Hata hivyo, bara hilo halifaidiki na utajiri wa aina hii.
Kulingana na tathmini ya Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF), mapato ya madini kama shaba, nickel, cobalt na lithium, yatagharimu jumla ya Dola trilioni 16 ndani ya miaka 25 ijayo, huku eneo la kusini mwa jangwa la Sahara likitarajia kuvuna zaidi ya asilimia 10 ya mapato haya.
Ni lazima tuitumie hii fursa kwa faida ya watu wetu.
Tatu, ni muhimu kuwa na fursa nyingi za kufanya biashara katika sekta ya nishati, hususani nishati jadidifu.
Bara la Afrika limejaliwa kuwa na aina nyingi za nishati hizi na zenye uwezo mkubwa.
Vilevile, ni muhimu kuimarisha uratibu katika usalama wetu.
Tunahitaji mfumo wa itajayokinga rasilimali zetu dhidi ya migogoro ya nje.
Hii ni pamoja kubadilishana taarifa za kigaidi ambazo zinaweza kuiga mifano ya yale yanayotokea Mashariki ya Kati.
Jambo la tano, ni umuhimu wa kuwekeza kwenye ustahimilivu wa kibinadamu.
Wakati ni sasa
Hatutakiwi kuwa watazamaji tu wakati mataifa yenye nguvu duniani yakija nna mifumo mipya.
Njia ya kufikia ustahimilivu, si njia rahisi japo ipo wazi.
Ni lazima tukuze biashara kati yetu wenyewe kwa kutumia sarafu zetu.
Kama tu Rais John Mahama alivyosema, “tuache kuongea tu, na tuanze kuchukua hatua”.
Kennedy Chileshe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Viongozi wa Jubilee, akiandikia kutoka Lusaka, Zambia.