| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Hichilema ashinda Uchaguzi wa Zambia
Ushindi huo umemuwezesha Hichilema kuvuka kizingiti cha kikatiba cha kupata zaidi ya asilimia 50.
Hichilema ashinda Uchaguzi wa Zambia
Hakainde Hichilema, amepata zaidi ya kura milioni 2. / / Reuters

Hakainde Hichilema ameshinda katika Uchaguzi Mkuu wa urais nchini Zambia baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu, Brian Mundubile, kwa zaidi ya kura milioni 1.1.

Hakainde Hichilema, amepata zaidi ya kura milioni 2.9 na hivyo kujihakikishia nafasi ya kuliongoza taifa hilo kwa muhula wa pili. Matokeo hayo ni kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia.

Brian Mundubile mpinzani kutoka Chama cha National Restoration Party for Unity and Progress (NRPUP), amepata kura milioni 1.8.

Ushindi huo umemuwezesha Hichilema kuvuka kizingiti cha kikatiba cha kupata zaidi ya asilimia 50.

“Tunawashukuru Wazambia. Kwa kweli tumeheshimiwa na kuaminiwa kwa kutukabidhi dhamana ya kuongoza ofisi ya juu kabisa ya nchi yetu na kuturuhusu kuwa watumishi wenu tena,” Hichilema amesema katika ujumbe aliouweka katika mtandao wa kijamii wa Facebook muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia, Mwanagala Zaloumis, kumtangaza kuwa rais mteule katika kituo cha kitaifa cha kutangazia matokeo jijini Lusaka, mji mkuu wa Zambia.

Zaloumis amesema Hichilema ameshinda kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba matokeo kutoka katika vituo maalumu vya kupigia kura vilivyosalia katika majimbo bunge matano kati ya majimbo bunge 226 ya nchi hiyo hayawezi kubadili kwa kiwango cha maana matokeo ya uchaguzi.

Mitaa ya Lusaka ilikuwa tayari imechangamka kabla hata ya kutangazwa rasmi kwa ushindi wa Hichilema, na iliendelea kuwa na shamrashamra kwa muda mrefu baadaye. Watu kutoka makundi mbalimbali ya jamii walijaa mitaani, wakivumilia hali ya hewa baridi mapema asubuhi kusherehekea ushindi huo.

“Mheshimiwa Rais, tafadhali endelea kuwa kiongozi mzuri kwa nchi hii. Watu wa Zambia wameonyesha tena imani na matumaini yao katika uongozi wako,” amesema Collins Maoma, Mwenyekiti wa Kitaifa wa chama kilichomsimamisha Hichilema, chama tawala cha United Party for National Development (UPND), alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

 

CHANZO:AA
Soma zaidi
Aliyekuwa afisa wa ujasusi Uganda arejeshwa Marekani kukabiliwa na mashtaka ya magendo
Mlipuko wa ugonjwa wa kimeta waua viboko 46 na tembo wanane nchini Zambia
Mwenge wa Olimpiki wawasili Senegal kwa ajili ya Olimpiki barani Afrika
Putin anaunga mkono juhudi za Afrika za kutaka mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Niger yamteua mkuu mpya wa jeshi baada ya jaribio la uasi lililozimwa
Mfalme Oyo Nyimba kuzikwa leo kwa mujibu wa mila na desturi
Putin na Ramaphosa wajadili uhusiano kati ya Urusi na Afrika Kusini katika mkutano wa BRICS
Rais wa Zimbabwe Mnangagwa atangaza siku yake ya kuzaliwa kuwa sikukuu ya kitaifa
Bunge la Nigeria lasitisha safari za wajumbe wake Afrika Kusini kufuatia vurugu dhidi ya wahamiaji
Uchaguzi wa Nigeria 2027: Tinubu vs Atiku
Algeria yaizuia UAE kutumia anga yake baada ya kusitisha uhusiano wa kidiplomasia
Mahakama yakataa ombi la Lissu kumuita Rais Samia kutoa ushahidi
Algeria yasitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na UAE
Ufalme wa Uganda wamteua mtangazaji wa televisheni kumrithi Mfalme Oyo Nyimba
Mufti Mkuu Tanzania atoa wito kwa Waislamu kufunga siku tatu kuomba kuepushwa na madhara ya El Nino
Umoja wa Mataifa wapongeza makubaliano ya Libya kuelekea katika uchaguzi
Putin amuambia Trump: Urusi haina nia ya kuzishambulia nchi za Ulaya
Wahamiaji zaidi ya 1,000 waokolewa pwani ya Afrika magharibi ndani ya wiki moja, MSF inasema
Ghana yasema imetumia $4.37 milioni kuwarudisha raia wake nyumbani kutoka Afrika Kusini
Waburundi waomba nyaraka za kusafiria kufuatia operesheni dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni Kenya