Filamu tatu zilizotayarishwa kwa ushirikiano na TRT zapigania tuzo ya 'Palme d’Or Cannes'

TRT inaendelea kuimarisha uwepo wake wa kimataifa katika sekta ya filamu, kazi zake zilizotayarishwa kwa ushirikiano na wakurugenzi mashuhuri duniani zapigania tuzo katika mashindano makuu ya Tamasha la Filamu la Cannes la 79.

By
Filamu tatu zilizotayarishwa kwa ushirikiano na TRT zapigania tuzo ya Palme d’Or Cannes / TRT World

Filamu tatu zilizotayarishwa kwa ushirikiano na TRT zinatarajiwa kushindania tuzo ya kifahari ya Palme d’Or katika Tamasha la Filamu la Cannes la 79.

Miradi hiyo inajumuisha kazi za wakurugenzi maarufu duniani Asghar Farhadi, Ryusuke Hamaguchi, na Andrey Zvyagintsev, jambo linaloonyesha kuongezeka kwa ushawishi wa TRT katika sinema ya kimataifa pamoja na dhamira yake ya kuendeleza uzalishaji wa kazi zenye ubora wa juu.

“Kushiriki katika miradi iliyosainiwa na wakurugenzi mashuhuri kama hawa kunaonyesha maono ya utangazaji ya TRT na nafasi yake kimataifa katika tasnia ya filamu,” alisema Mkuu wa Mawasiliano wa Uturuki, Burhanettin Duran.

“Tunawapongeza wote waliohusika katika utayarishajishaji huu mzuri na tunazitakia filamu zetu kila la heri katika safari ya kuelekea Palme d’Or.”

Kwa kuendelea kuimarisha uwezo wake wa kushiriki katika utayarishaji wa pamoja na kuunga mkono miradi ya kipekee, TRT inaendelea kujikita kama mdau muhimu katika sinema ya kimataifa.