Rais Mwinyi wa Zanzibar ataka wananchi waelimishwe kuhusu umuhimu wa tafiti

Rais Mwinyi wa Zanzibar ameshauri kuangaliwa upya kwa sera, sheria na kanuni katika eneo hilo.

By
Rais Mwinyi ameshauri kuangaliwa upya kwa sera, sheria na kanuni katika eneo hilo. Picha/Ikulu Zanzibar. / TRT Afrika Swahili

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameushauri uongozi wa Kituo cha Tafiti za Kiuchumi, Kijamii na Uchambuzi wa Sera Zanzibar (ZRCP) kuandaa mikutano na mijadala na wadau ili kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kutumia matokeo ya tafiti katika utekelezaji wa majukumu yao.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, Machi 24, 2026, alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho, Juma Reli, pamoja na ujumbe wake waliofika Ikulu, Zanzibar.

Aidha, amebainisha umuhimu wa kufanya maboresho katika mifumo ya usajili wa malipo ya kidijitali ili kuimarisha muda na uwazi, hususan katika sekta ya umma, na kushauri kuangaliwa upya kwa sera, sheria na kanuni katika eneo hilo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa ZRCP, Juma Hassan Reli, ameunga mkono mapendekezo hayo na kueleza kuwa kituo hicho kipo tayari kushirikiana na Serikali katika kutoa tafiti na mapendekezo yatakayochangia maboresho ya mifumo ya malipo ya kidijitali, ikiwa ni pamoja na kusaidia mapitio ya sera, sheria na kanuni ili kuimarisha uwazi na ufanisi katika sekta ya umma.