Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amekuwa mwenyeji wa Kansela wa Austria, Christian Stocker jijini Ankara siku ya Jumatatu.
Stocker yupo nchini Uturuki kwa mwaliko wa Rais Erdogan.
Kati ya mambo yatakayojadiliwa wakati wa mkutano huo, ni pamoja ni namna ya kuendeleza ushirikiano, mambo ya kikanda na ya kiulimwengu.
Katika siku za karibuni, ushirikiano mataifa hayo, umezidi kuimarika huku pande zote zikionesha nia ya kuendelea kushirikiana kupitia biashara,uhamiaji na usalama.
Aprili mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan aliitembelea Austria, ambako alikutana na waziri mwenzake, Beate Meinl-Reisinger pamoja na Kansela Stocker, wakiashiria nia ya kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo, pamoja na kujadili migogoro ya kikanda.
Kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, ujazo wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, ulifikia Dola bilioni 4.36 mwaka 2025 kutoka Dola bilioni 3.91, mwaka 2024.





















