| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
IMF yaipatia Tanzania Dola milioni 443.9
IMF imeeleza kuwa uchumi wa Tanzania umeendelea kuonyesha uimara, huku ukuaji wa Pato la Taifa ukifikia asilimia 5.9 mwaka 2025 na kutarajiwa kufika karibu asilimia 6.2 kwa muda wa kati.
IMF yaipatia Tanzania Dola milioni 443.9
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania / Reuters

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), limeidhinisha kutolewa mara moja kwa takriban dola za Marekani milioni 443.9 kwa Tanzania baada ya kukamilisha tathmini za mwisho chini ya programu za Extended Credit Facility (ECF) inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii na Resilience and Sustainability Facility (RSF) ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

 Katika taarifa iliyotolewa Julai 10, IMF imesema uamuzi huo unafuatia kukamilika kwa mapitio ya sita na saba ya mpango wa ECF pamoja na mapitio ya tatu na nne ya mpango wa RSF, ambapo fedha hizo zinajumuisha takriban dola za Marekani milioni 158.75 chini ya ECF na Dola za Marekani milioni 298.37 chini ya RSF.

IMF imeeleza kuwa uchumi wa Tanzania umeendelea kuonesha uimara, huku ukuaji wa Pato la Taifa ukifikia asilimia 5.9 mwaka 2025 na kutarajiwa kufika karibu asilimia 6.2 kwa muda wa kati. Sekta zilizotajwa kuchangia matarajio hayo ni pamoja na madini, kilimo na utalii.

Kwa mujibu wa tathmini hiyo, Tanzania imeendelea kudumisha utulivu wa uchumi mpana na mfumuko wa bei umebaki chini, ukiwa asilimia 4.0 mwezi Juni 2026. Hata hivyo, IMF imeonya kuwa kupanda kwa bei za mafuta duniani kunaendelea kutoa shinikizo kwa gharama za maisha na uchumi kwa ujumla.

Taarifa hiyo imeonesha pia kuwa utekelezaji wa mpango wa mageuzi ya kiuchumi kwa ujumla ulikuwa wa kuridhisha. Vigezo vingi vya utendaji vilifikiwa kwa wakati, ingawa baadhi ya malengo na mageuzi, hasa katika maeneo ya nishati, usimamizi wa VAT, utawala wa Benki Kuu na uwekezaji wa umma, yalichelewa au hayakukamilika kama ilivyotarajiwa.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Umoja wa Mataifa wapongeza makubaliano ya Libya kuelekea katika uchaguzi
Putin amuambia Trump: Urusi haina nia ya kuzishambulia nchi za Ulaya
Wahamiaji zaidi ya 1,000 waokolewa pwani ya Afrika magharibi ndani ya wiki moja, MSF inasema
Ghana yasema imetumia $4.37 milioni kuwarudisha raia wake nyumbani kutoka Afrika Kusini
Waburundi waomba nyaraka za kusafiria kufuatia operesheni dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni Kenya
Watu wawili wafariki, wengine 25 wajeruhiwa baada ya basi la mahujaji wa Misri kupata ajali Makkah
Mume wa Rais Samia wa Tanzania afariki dunia
Cabo Verde yatangaza maombolezo ya kitaifa baada ya vifo vya watoto katika ajali ya basi
Mlipuko wa kipindupindu, Kordofan Magharibi umesababisha vifo vya watu 23
Romanda Hombir wa Afrika Kusini ashinda taji la Miss World Africa 2026
DRC inachunguza ajali mbaya ya moto katika sherehe ya harusi ulioua wageni 22
Unyanyasaji kwa wazee janga linaloenea kimya kimya
Marekani kuondoa ufadhili wa Dola milioni 45 za VVU kwa Namibia
Niger yaishutumu Ufaransa kwa jaribio lililofeli la uasi wa kijeshi
Huduma ya Kitaifa ya Polisi ya Kenya (NPS) inatoa onyo kwa wanasiasa kabla ya uchaguzi mkuu
Marekani yaongeza muda wa AGOA hadi mwisho wa 2028
Marekani inashinikiza kusitishwa kwa mapigano kwa sababu za kibinadamu bila vikwazo nchini Sudan
UN yapiga kura kuidhinisha ramani ya dunia inayoonyesha ukubwa halisi wa Afrika
Mfalme Oyo Nyimba: Mwili wa mfalme mdogo zaidi warudishwa Uganda kwa mazishi
Raia wa Marekani waokolewa baada ya mashambulizi katika kambi ya mbuga ya wanyamapori Msumbiji