| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan: Kwa Israel kutambua Somaliland hakutamfaidi yeyote
Nchi katika kanda lazima zitafute suluhu wenyewe kwa matatizo yanayokumba kanda, Erdogan amesema wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy jijini Addis Ababa.
Erdogan: Kwa Israel kutambua Somaliland hakutamfaidi yeyote
Rais Recep Tayyip Erdogan na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Addis Ababa Februari 17, 2026. / AA
17 Februari 2026

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan siku ya Jumanne alizungumzia kuhusu uamuzi wa israel kuitambua Somaliland kama taifa huru na ikiwa nchi pekee iliyofanya hivyo, akisisitiza kuwa uamuzi huo hautofaidi Somalia wala kanda hiyo.

"Ningependa kusisitiza kuwa kwa Israel kutambua Somaliland hakutafaidi Somaliland wala Pembe ya Afrika," Erdogan amesema katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed jijini Addis Ababa.

Uturuki inaamini kuwa nchi katika kanda hii zinatakiwa kutafuta suluhu ya matatizo ya katika kanda yao wenyewe, amesema Erdogan, akitoa wito kwa Pembe ya Afrika kutogeuzwa "kuwa sehemu ya malumbano ya mataifa ya nje.”

Akisisitiza kuhusu ushirikiano kati ya Uturuki na Ethiopia, Erdogan amesema kuwa ni "fahari kubwa" kuwa makampuni zaidi ya 200 ya Uturuki, yenye uwekezaji wa dola bilioni $2.5, yanasaidia kutoa ajira kwa watu karibu 20,000 nchini Ethiopia.

‘Nia ya kufikia bahari’

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu wa ​​​​​​​Ethiopia amesema kuwa ameiomba Uturuki iwasaidie katika mchakato wao wa kutaka kutumia bahari, akieleza hilo kuwa eneo la msingi watakaloangazia katika mazungumzo yao na rais wa Uturuki.

Abiy alisema katika mkutano huo wa pamoja na waandishi wa habari kuwa alijadili nia ya Ethiopia ya kutaka “kufikia bahari” na kiongozi wa Uturuki na kupongeza majadiliano muhimu na yenye tija kuhusu suala hilo.

Ethiopia, ambayo ni nchi isiyokuwa na bahari tangu uhuru wa Eritrea 1993, imekuwa ikieleza kuwa kufikia bahari kama suala la kipaumbele kimkakati.

Ziara ya Erdogan ni ishara ya ziara ya ngazi ya juu ikiwajumuisha mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa Uturuki, miongoni mwa wengine, na imekuja wakati nchi hizo mbili zikitaka kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa hasa wakiadhimisha karne moja ya ushirikiano ulioanza 1926.

Viongozi hao walijadili kupanua ushirikiano wao wa kibiashara,huku maafisa wa Ethiopia wakisema pande zote mbili zinataka kuongeza kiwango cha biashara kisiwe chini ya dola bilioni $1.

Abiy pia alihimiza uwekezaji zaidi wa makampuni ya Uturuki nchini Ethiopia, nchi ambayo tayari ina mkusanyiko mkubwa zaidi wa wafanyabiashara wa Uturuki Kusini mwa jangwa la Sahara, hasa katika sekta ya viwanda na ujenzi.

Pande zote mbili pia zilijadili ushirikiano katika majukwaa ya kimataifa, ikiwemo majadiliano yanayohusiana na COP31, ambayo itafanyika nchini Uturuki, alafu mkutano unaofuata ufanyike nchini Ethiopia mwakani.

CHANZO:AA
Soma zaidi
Kalin wa Uturuku awapokea wajumbe wa Hamas kujadili mpango wa amani wa Gaza
Ikiongozwa na Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan, dunia inaadhimisha Siku ya taka sufuri
Stratcom 2026 inakamilika mjini Istanbul kwa wito wa mawasiliano yanayotegemea ukweli
Vita vya Israel na Marekani dhidi ya Iran vinahatarisha mzozo wa kikanda: Mkuu wa ujasusi wa Uturuki
Fidan wa Uturuki: Vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran ni “kinyume cha sheria”
Vita visivyo na maana Mashariki ya Kati vinaathiri binadamu wote: Erdogan
Mkutano wa Stratcom 2026 wafunguliwa Istanbul wakati mvutano wa kimataifa ukiongezeka
Rais Erdogan atadhaharisha mfumo wa baada ya Vita ya Pili ya Dunia kupoteza uhalali wake
Uturuki haitokaa kimya wakati Israel inalitumbikiza eneo zima katika umwagaji damu: Erdogan
Hakan Fidan wa Uturuki aongoza juhudi za kusitisha vita vya Mashiriki ya Kati
Rais wa Uturuki na mwenzake wa Kazakhstan wajadili uhusiano wa mataifa mawili, masuala ya kikanda
Uturuki imeazimia kubaki mbali na mzozo hatari unaoendelea: Erdogan
Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan aadhimisha Siku ya Maji Duniani, atahadharisha uhaba wa maji
Rais Erdogan atarajia Nowruz italeta amani Mashariki ya Kati
Rais wa Uturuki ahimiza umoja wakati wa Eid al-Fitr huku kukiwa na mvutano wa Mashariki ya Kati
Uturuki inashikilia msimamo thabiti juu ya ukiukaji wa anga, inaimarisha usalama wa taifa: Erdogan
Viongozi wa Uturuki na Oman wajadili kuongezeka kwa mvutano wa kikanda huku kukiwa na vita vya Iran
Mfumo wa ziada wa Patriot wa NATO kupelekwa Adana Uturuki, wizara ya ulinzi inasema
Uturuki inasukuma kugeuza Sahel kuwa eneo la ulinzi la Afrika katika maonyesho ya BAMEX 2026
Rais Erdogan aadhimisha Ushindi wa Vita vya Dunia vya Kwanza vya Canakkale