Trump: Marekani ina "nguvu kubwa" inayoelekea Iran

Tuna msafara mkubwa unaoelekea huko, labda hatutahitaji kuutumia. Tutaona, anasema Rais wa Marekani.

By
Trump alisema kwamba Marekani inaifuatilia Iran kwa karibu. / AP

Rais wa Marekani Donald Trump alisema Alhamisi kuwa kuna "nguvu kubwa" inayoelekea Iran.

"Mnajua, tuna meli nyingi zinazoelekea upande huo, kwa tahadhari. Tuna meli kubwa (zinazoelekea) upande huo na tutaona kitakachotokea," aliwaambia waandishi wa habari akiwa katika Air Force One akielekea Washington kutoka Davos, Uswisi.

"Tuna nguvu kubwa inayoelekea Iran. Ningependa nisione jambo lolote litokee."

Trump alisema kuwa Marekani 'inafuata Iran kwa umakini mkubwa.'

"Tuna armada. Tuna meli kubwa zinazokwenda upande huo na huenda hatutahitaji kuzitumia. Tutaona," alisisitiza.

Kwa upande wake, Iran kwa mara nyengine imeitahadharisha Marekani na Israel dhidi ya hatua zozote za kijeshi, na kusema kuwa vikosi vyake vimejiandaa kwa lolote.

Jenerali Mohammad Pakpour amesema raia wa Iran and wamejiandaa kutekeleza amri yoyote itakayotoka kwa Kiongozi Mkuu Ali Khamenei. Jenerali mwengine ametahadharisha kwamba iwapo Marekani itashambulia, "basi washirika wote wa marekani, ikiwemo kambi" yatakuwa ni maeneo halali ya kulengwa.