Idadi ya Waislamu ulimwenguni, huenda ikaizidi ili ya Wakristo, kufikia mwaka 2035, kulingana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya Pew, kuhusu mustakabali wa dini duniani.
Utafiti huo, wenye kuangazia ongezeko la waamini wa makundi saba ya kiimani duniani, kati ya mwaka 2020 na 2070, umebaini kuwa wafuasi wa dini zote wanaongezeka, japo kundi la Waislamu linaongezeka zaidi.
Kulingana na utafiti huo, idadi ya Waislamu inakadiriwa kufikia zaidi ya bilioni 3.6, huku ile ya Wakristo ikiwa ni bilioni 3, ifikapo mwaka 2070.
Wakati huo huo, idadi ya watu duniani inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 29 katika kipindi hicho.
Ripoti hiyo, inaeleza kuwa, waamini wa Kiislamu watachangia asilimia 36 ya idadi ya watu duniani, huku ya Wakristo ikiwa ni asilimia 29, ifikapo mwaka huo.
Ongezeko kubwa, linatarajiwa kushuhudiwa katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambapo kuna idadi kubwa ya Wakristo na Waislamu.




















