Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imelaani vikali shambulizi lililofanywa na vikosi vya RSF vya nchini Sudan, kwenye gari lililokuwa limebaba watu wasio na makazi, katika eneo la Jimbo la Kordofan.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, tukio hilo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu na ulinzi wa uhai wa binadamu na mali zao.
“Tumesikitishwa na vifo vya watu wengi kufutia shambulizi lililofanywa na RSF, likilenga gari lililokuwa limebeba awatu wasio na makazi,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Vile vile, Uturuki imelaani vikali mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia, ikitaka kuwepo na ulinzi wakati wa kusafirisha binadamu na misaada kwenye maeneo yaliyokumbwa na machafuko.
Februari 7, shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani ya wapiganaji wa Sudan, lililenga gari lililokuwa limebeba familia zilizokuwa zimeondoka kwenye makazi yao katikati mwa Sudan, kuua watu wasiopungua 24, ikiwemo watoto wanane, kulingana na taasisi moja ya madaktari.
Shambulio hilo lilitokea karibu na mji wa Rahad, katika jimbo la Kordofan Kaskazini.
Gari hilo lililokuwa likisafirisha watu waliokimbia makazi yao kutokana na vita huko eneo la Dubeiker Kordofan Kaskazini.
Miongoni mwa waliofariki walikuwa watoto wawili wachanga.

























