| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Sudan Kusini kufanya Uchaguzi Mkuu Disemba 22
Kulingana na maofisa wa tume ya uchaguzi wa nchi hiyo, usajili wa wapiga kura unategemewa kuanza hivi karibuni.
Sudan Kusini kufanya Uchaguzi Mkuu Disemba 22
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini./Picha:Reuters / Reuters

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Sudan Kusini imetenga Disemba 22, 2026 kama siku ya kufanya Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Kulingana na Mwenyekiti wa Tume ya NEC ya Sudan Kusini Abednego Akok Kacuol, siku hiyo inaenda sanjari na Sheria ya Uchaguzi wa nchi hiyo  na mchakato wa upatikanaji wa amani ambao unafikia kikomo Disemba 2026.

"Uchaguzi utafanyika Disemba 22, 2026 kama ilivyoainishwa kwenye sheria ya uchaguzi,” alisema  Akok katika mkutano wake na wanahabari siku ya Jumatatu.

Disemba 2024, serikali ya mpito ya umoja wa taifa, iliongeza muda wake kutoka Disemba 22, 2024, hadi Disemba 22, 2026.

 

CHANZO:AA