| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Wahamiaji wapatao 160 waokolewa baada ya meli yao kuwaka moto
Kwa muda mrefu sasa, Ufaransa imegeuka kuwa kivuko cha wahamiaji, wenye ndoto za kwenda kutafuta maisha nchini Uingereza.
Wahamiaji wapatao 160 waokolewa baada ya meli yao kuwaka moto
Kwa muda mrefu sasa, Ufaransa imegeuka kuwa kivuko cha wahamiaji, wenye ndoto za kwenda kutafuta maisha nchini Uingereza.

Vikosi vya uokoaji vya Ufaransa na Uingereza, vimeokoa wahamiaji 157, baada ya meli ya kushika moto, wakati ikivuka eneo la bahari linalotenganisha kusini mwa Uingereza na kaskazini mwa Ufaransa.

"Boti ndogo ilishika mota kati eneo hilo la mfereji wa nchi hizo mbili na kuwalazimu abiria waanze kujitosa baharini,” ilisema sehemu ya taarifa ya mkuu wa eneo la Pas-de-Calais, siku ya Jumanne.

Kwa muda mrefu sasa, Ufaransa imegeuka kuwa kivuko cha wahamiaji, wenye ndoto za kwenda kutafuta maisha nchini Uingereza.

Wahamiaji hao, wanadaiwa kulipa fedha nyingi kwa madalali maalumu, ili kuvuka kuelekea upande wa pili.

Zaidi ya wahamiaji 41,000 waliwasili kusini mwa pwani ya Uingereza mwaka jana, ikiwa ni idadi ya juu zaidi kwa mwaka, tangu 2018.

Mwaka huu peke yake, watu 14 wanaripotiwa kupoteza maisha wakati wakijaribu kuvuka mfereji huo.

CHANZO:AFP