| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Putin wa Urusi aunga mkono azma ya Afrika kuwa na nafasi za kudumu Umoja wa Mataifa
Rais Putin anasema Urusi inaunga mkono azma ya Afrika ya kuwa na nafasi za kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Putin wa Urusi aunga mkono azma ya Afrika kuwa na nafasi za kudumu Umoja wa Mataifa
Viongozi zaidi ya 20 wa Afrika wamehudhuria Kongamano la 3 la Urusi na Afrika jijini Moscow kuanzia tarehe 28 hadi 29 Oktoba 2026. / Reuters

Azma ya Afrika kupata nafasi za kudumu ndani ya Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa imeungwa mkono na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Hili linakuja wakati viongozi zaidi ya 20 wa Afrika wakiwa jijini Moscow kwa Kongamano la 3 la Urusi na Afrika lililofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 29 Oktoba.

Putin anasema Urusi inafanya ‘’kila iwezalo’’ kuipa uwezo Afrika duniani na kuhakikisha ‘’kuna uwakilishi wa sawa’’ katika Baraza la Usalama na kwa taasisi za kimataifa za fedha.

Alizungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye pembeni mwa mkutano huo, ambapo masuala ya biashara na usalama pia yalijadiliwa.

Mataifa 5 yanatofautiana kuhusu uwezekano wa nafasi za Afrika

Kiongozi huyo wa Urusi alishtumu kile alichokiita ‘ukoloni mamboleo’ wa nchi za Magharibi barani Afrika licha ya mtazamo wa kisiasa kubadilika.

Rais wa Burundi Ndayishimiye, ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, alimshkuru Putin kwa kuunga mkono uwakilishi wa kudumu wa Afrika kwenye Baraza hilo, akisema kuwa kutasaidia kuhakikisha ‘’mfumo wa haki na demokrasia duniani’’.

Afrika inahitaji kuwa na nafasi za kudumu na usawa wa kura ya turufu ambao umekuwa ukifaidi mataifa matano ya sasa ya kudumu tangu mwaka 1945 – Marekani, Uingereza, Urusi, Ufaransa na China.

Nchi zote tano zimeunga mkono azma ya Afrika kuwa na nafasi za kudumu, lakini wanatofautiana kuhusu utaratibu.

Ufaransa inaunga mkono kuwepo kwa nafasi za kudumu na uwezo wa kura ya turufu, Marekani na Uingereza inaunga mkono kuwepo kwa nafasi hizo bila uwezo wa kura ya turufu, Urusi na China inaunga mkono nafasi hizo ila hazijazungumza chochote kuhusu kura ya turufu.

CHANZO:TRT Afrika Swahili