Serikali ya Tanzania, kupitia Msemaji wake Mkuu, Gerson Msigwa, imeeleza kusikitishwa kwake na makala ya BBC Africa Eye, kwa madai ya kuchapitishwa bila kutoa nafasi kwa viongozi na maafisa wa serikali kujibu baadhi ya tuhuma zilizoibuliwa.
Msingwa alisema kuwa makala hiyo imejenga picha mbaya kwa nchi bila serikali kupewa nafasi sawa ya kusikilizwa kama inavyotakiwa katika msingi wa taaluma ya uandishi wa habari.
Amesema kuwa serikali inafanya tathmini ya makala hiyo na kuahidi kuchukuliwa kwa hatua stahiki za kulinda heshima, uhuru, na usalama wa nchi dhidi ya upotoshaji.
Julai 13, BBC Africa Eye ilichapisha makala inayoangazia hali ya kisiasa na demokrasia nchini Tanzania. Huku ikiangazia kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu.
Mpaka sasa BBC Africa Eye haijatoa ufafanuzi wowote kuhusu kauli hiyo ya serikali.
Wakati huo huo, kumekuwa na shinikizo kutoka kwa wadau mbalimbali wakiitaka serikali kumuachia Lissu, ambae amekuwa kizuizini tangu Aprili 2025, kwa tuhuma za uhaini, ambazo mwenyewe amezikana.
AFRIKA
1 dk kusoma
Serikali ya Tanzania yasikitishwa na makala ya BBC Africa Eye
Msingwa alisema kuwa makala hiyo imejenga picha mbaya kwa nchi bila serikali kupewa nafasi sawa ya kusikilizwa kama inavyotakiwa katika msingi wa taaluma ya uandishi wa habari.

Soma zaidi













