Kituo maarufu cha hija ya Wakatoliki nchini Bosnia, kimeharibu vibaya, siku chache kabla ya maelfu ya mahujaji kutembelea kituo hicho.
Kituo cha Marian wa Medjugorje, kilichopo kilomita 140, kusinimagharibi mwa jiji la Sarajevo, kilianza kupata umaarufu kwenye miaka ya 1980, baada ya kuripotiwa kutokea kwa Bikira Maria, kwa watoto sita wa eneo hilo.
Vyombo vya habari nchini Bosnia, vilionesha uharibifu mkubwa wa eneo hilo, ikiwemo sanamu ya Bikira Maria, ikiwa rangi nyeusi iliyopulizwa kwenye uso wa Bikira Maria.
Kamera za usalama, zilimuonesha mtu mmoja akiiwasha altare ya kituo hicho cha hija moto, karibu na Kanisa la Mtakatifu Yakobo.
Tukio hilo limetokea siku chache, kabla ya ibada ya hija ambayo hufanyika wiki ya kwanza ya mwezi wa nane, na kuhudhuriwa na zaidi ya vijana 50,000 kutoka sehemu mbali mbali duniani.
Miaka miwili iliyopita, Vatican ilikitambua kituo hicho, ambacho kinaendelea kujipatia umaarufu na kuvutia mahujaji wengi kila mwaka.


















