Waziri Mkuu wa Ethiopia ataka mafuta yahifadhiwe, mgogoro wa Mashariki ya Kati ukiendelea
Abiy Ahmed amewataka wasambazaji wa nishati hiyo kuweka kipaumbele kwenye uhifadhi wa mafuta katika kipindi cha mgogoro wa Mashariki ya Kati.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amewataka wasambazaji na watumiaji wa mafuta kuhifadhi nishati hiyo muhimu wakati ambapo mgogoro katika eneo la Mashariki ya Kati ukiathiri upatikanaji wa nishati hiyo.
Kulingana na Abiy, mgogoro huo umechelewesha upatikanaji wa mafuta, hususan katika mataifa yanayotegemea zaidi nishati hiyo, ikiwemo Ethiopia.
“Kwa kuzingatia yanayoendelea huko Mashariki ya Kati, mataifa yenye kununua bidhaa za mafuta sasa yanapata taabu kupata mafuta kama ilivyo kawaida,” alisema Abiy kupitia taarifa yake kwenye mtandao wa X.
“Mpaka pale tatizo hilo likitatuliwa, hali itarejea kawaida,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Abiy amewataka wasambazaji wa mafuta na wamiliki wa vituo vya mafuta pamoja na watumiaji, kuielekeza bidhaa hiyo kwenye huduma nyingine muhimu kama vile usafiri, afya vyakula na kadhalika.