Kardinali McElroy wa Marekani alaani vita dhidi ya Iran

Kardinali McElroy alisema kuwa vita hivyo havipaswi kuendelea, huku akisisitiza kuwa sababu za Marekani kuivamia Iran, bado hazieleweki.

By
Siku chache zilizopita, Blaise Kardinali Cupich, alisikitishwa na picha mjongeo mmoja iliyochapishwa na Ikulu ya Marekani./Picha:Wengine

Robert Kardinali McElroy, ambaye pia Askofu Mkuu wa Washington, amesema mashambulizi yanayofanywa na Marekani dhidi ya Iran hayakubaliki.

Katika mahojiano yake na jarida la Catholic Standard linalomilikiwa na Jimbo la Washington, kardinali McElroy alisema kuwa vita hivyo ni haramu kulingana na mafundisho na imani ya Kikatoliki.

"Kama Papa Benedikto alivyosema, Kanisa Katoliki haliruhusu vita vya namna hii," alisema katika mahojiano hayo yaliyochapishwa siku ya Jumatatu.

Kardinali McElroy alisema kuwa vita hivyo havipaswi kuendelea, huku akisisitiza kuwa sababu za Marekani kuivamia Iran, bado hazieleweki.

"Nchi yetu imekuwa mhanga wa vita kama hivi huko nyuma, hususani katika eneo la Mashariki ya Kati," alieleza.

Siku chache zilizopita, Blaise Kardinali Cupich, alisikitishwa na picha mjongeo mmoja iliyochapishwa na Ikulu ya Marekani, ikiwa na wahusika wa Hollywood.

Maoni ya makardinali hao wawili, yanakuja huku Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, kushindwa kulaani moja kwa moja, mashambulizi ya Marekani-Israel dhidi ya Iran.