| swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Msongamano katika mazishi ya Raila wasababisha watu kadhaa kujeruhiwa
Watu kumi na nane wamejeruhiwa wakati wa msongamano uliojitokeza katika uwanja wa Nyayo wakati wa mazishi ya kitaifa ya Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, aliyefariki dunia wiki hii India akiwa na umri wa miaka 80.
Msongamano katika mazishi ya Raila wasababisha watu kadhaa kujeruhiwa
Msongamano ulitokea katika uwanja wa Nyayo uliopo jijini Nairobi, wakati umma ulipokuwa ukiuaga mwili wa Odinga.
17 Oktoba 2025

Wakenya wamejitokeza kwa wingi kuomboleza kifo cha Odinga tangu alipoaga dunia Jumatano, jambo linaloonyesha ushawishi mkubwa wa kiongozi huyo aliyeheshimiwa katika siasa za nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Msongamano ulitokea katika uwanja huo uliopo jijini Nairobi, wakati umma ulipokuwa ukiuaga mwili wa Odinga.

Shirika la Msalaba Mwekundu wa Kenya limesema tukio hilo "lilisababisha watu wengi kuhitaji huduma za dharura." Chanzo katika hospitali kuu ya rufaa nchini kilisema walipokea watu 18 waliokuwa wamejeruhiwa.

Maelfu ya watu wamejaza uwanja wa Nyayo ambapo jeneza la Odinga lilifunikwa na bendera ya taifa kwa ajili ya ibada ya Kanisa la Anglican. Watu walikuwa wakimwimbia nyimbo na kuonyesha picha za Odinga, huku wengine wakibeba matawi, ambayo ni ishara ya amani na mshikamano katika mila za Kenya.

Kulikuwa na usalama mkali uwanjani baada ya watu wanne kuripotiwa kufariki dunia wakati wa kuuaga mwili wa Odinga siku ya Alhamisi, wakati polisi walipojaribu kudhibiti umati mkubwa katika uwanja Kasarani.

Angalau watu 10 walijeruhiwa katika tukio la Alhamisi baada ya polisi kufyatua risasi na kutumia mabomu ya machozi dhidi ya umati uliokuwa ukijaribu kufikia eneo la jeneza.

CHANZO:AP
Soma zaidi
UN yaagiza uchunguzi wa dharura ufanyike kuhusu ukiukaji wa sheria katika Al Fasher ya Sudan
Rais wa Tanzania atangaza uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji katika uchaguzi
Wakimbizi 57,000 wamewasili kaskazini mwa Sudan baada ya mashambulizi ya RSF huko Darfur, Kordofan
Afrika Kusini yaruhusu kuingia kwa wakimbizi zaidi ya 150 kutoka Gaza, Palestina
Afrika yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu mbaya zaidi katika miaka 25
Mataifa ya G7 walaani mashambulizi ya RSF dhidi ya raia Sudan, watoa wito wa kusitishwa mapigano
Wakenya zaidi ya 200 wajiunga na jeshi la Urusi
AU yakanusha tuhuma za Trump kuhusu mauaji ya halaiki Nigeria
Mwigulu Nchemba ateuliwa Waziri Mkuu Tanzania
Jaji Mkenya achaguliwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amfuta kazi makamu wake
Duma wa Botswana aipa India zawadi ya duma 8
Kesi ya Roger Lumbala wa DRC yaanza kusikilizwa
Kesi za ubakaji, watoto kupotea zaripotiwa Darfur, Sudan – Umoja wa Mataifa
Ugonjwa wa Kichaa cha mbwa barani Afrika: Janga linaloendelea kuathiri maisha japo linaepukika
Libya yatakiwa kufunga vituo vya kuwazuilia wahamiaji katika mkutano wa Umoja wa Mataifa
Rais Museveni aonya kuzuka kwa vita endapo nchi za Afrika zitashindwa kufikia Bahari ya Hindi
UN: Milioni 11 wanawake na wasichana wanabeba uzito mkubwa wakati njaa ya Sudan inaendelea kupamba moto
Ethiopia yachagguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, COP32
Ghana yafichua sababu ya ajali ya helikopta iliyoua watu wanane, wakiwemo mawaziri, mwezi Agosti