Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA), Gianni Infantino, ameliomba radhi baraza la shirikisho hilo, kuhusiana na mpango wake wa awali wa kutaka kuuza haki za Kombe la Dunia.
Infantino, alichukua uamuzi huo, siku ya Alhamisi wakati wa mkutano uliofanyika jijini Zurich, Uswisi.
Kupitia mpango wa FIFA Forward Enterprise (FFE), Infantino alikuwa amelenga kuhamisha sehemu ya haki za kibiashara za FIFA kwa kampuni binafsi ya uwekezaji, huku thamani ya shirikisho hilo, ikitajwa kuwa karibu dola bilioni 20.
Miongoni mwa wawekezaji wakuu waliotajwa alikuwa Thrive Eternal, kampuni ya uwekezaji ya mwekezaji wa mitaji ya ubia Joshua Kushner, ambaye ni kaka wa Jared Kushner, mkwe wa Rais wa Marekani Donald Trump.
Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wa Baraza la FIFA wamesema msamaha huo haujajibu maswali muhimu yaliyopo.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha England (FA) na Makamu Rais wa FIFA, Debbie Hewitt, alisisitiza kuwa, Infantino anapaswa kuweka wazi nyaraka zote zinazohusiana na mpango huo na kutoa majibu ya kina kuhusu masuala yaliyozua utata.
MICHEZO
1 dk kusoma
Infantino aomba radhi kuhusu mpango wa kubinafsisha haki za kibiashara za FIFA
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la FIFA wamesema msamaha huo haujajibu maswali muhimu yaliyopo.
Soma zaidi



















