| Swahili
MICHEZO
2 dk kusoma
FIFA yawaadhibu wachezaji wa Argentina, yaitoza faini shirikisho kwa matukio ya Kombe la Dunia
Leandro Paredes amepewa marufuku ya mechi 10 wakati shirikisho hilo la dunia likikemea matukio ya baada ya kumalizika kwa mechi ya fainali, na bango la Falklands
FIFA yawaadhibu wachezaji wa Argentina, yaitoza faini shirikisho kwa matukio ya Kombe la Dunia
Mvutano kati ya wachezaji wa Argentina na Hispania baada ya mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2026.

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) siku ya Ijumaa lililitoza faini Shirikisho la Soka la Argentina (AFA) na kuwapa marufuku ya mechi kadhaa wachezaji watatu na afisa mmoja wa benchi la ufundi kwa yaliyotokea wakati wa fainali ya Kombe la Dunia 2026, ikiwemo vuta nikuvute ya baada ya fainali hiyo dhidi ya Hispania.

Kiungo wa Argentina Leandro Paredes alipewa marufuku ya mechi 10 na Kamati ya Nidhamu ya FIFA na kutozwa faini ya $90,000.

Mchezaji wa safu ya ulinzi Nahuel Molina atakuwa nje kwa michezo saba na kutozwa faini ya fedha kama hizo, huku kiungo Thiago Almada akipewa marufuku ya mechi moja na faini ya $30,000.

Kocha msaidizi wa Argentina Roberto Ayala atatumikia marufuku ya mechi tatu na kutakiwa kulipa faini ya $30,000.

Kiungo wa Hispania alipewa marufuku ya mechi moja na faini ya $30,000 kwa kuhusika katika tukio hilo.

Marufuku hiyo inafuatia mtafaruku uliotokea baada ya Hispania kuifunga Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia nchini Marekani mwezi uliopita.

FIFA pia iliitoza faini ya $321,000 AFA kutokana na ukiukwaji wa nidhamu wakati wa mashindano hayo, ikiwemo kuonesha bango lenye ujumbe unaohusisha Visiwa vinavyozozaniwa vya Falkland, pia vinavyojulikana kama Malvinas nchini Argentina, wakati wa mechi ya nusu fainali dhidi ya England.

Miongoni mwa faini hizo, $100,000 itawekezwa katika mipango dhidi ya ubaguzi wa rangi, huku $100,000 ikiwa itatozwa tu pale masharti yatakapokiukwa katika kipindi cha uangalizi.

Argentina pia ilitakiwa kucheza mechi zake mbili zinazokuja za nyumbani wakiwa na mashabiki nusu uwanja.

FIFA ilisema hayo yanahusishwa na ukiukwaji ikiwemo “kutumia michezo kwa maandamano yasiyohusiana na masuala michezo,” ubaguzi, utovu wa nidhamu na kukiuka utaratibu wa usalama.

Shirikisho hilo la soka duniani linasema maamuzi hayo yamefuata mchakato wa nidhamu kutokana na matukio ya wakati wa Kombe la Dunia na walioadhibiwa wana fursa ya kukata rufaa iwapo watataka kufanya hivyo.

CHANZO:َAA