| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan atoa wito wa kuendeleza mazungumzo ya Istanbul ili kumaliza vita vya Urusi na Ukraine
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameeleza kuwa Ankara iko tayari kujadili na Urusi "mapendekezo yoyote yanayoweza kuharakisha kusitishwa kwa mapigano, na kuweka msingi wa amani ya haki na ya kudumu."
Erdogan atoa wito wa kuendeleza mazungumzo ya Istanbul ili kumaliza vita vya Urusi na Ukraine
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wakizungumza na waandishi wa habari jijini Ankara. / AA
19 Novemba 2025

Uturuki inaamini mchakato wa Istanbul kuhusu vita vya Ukraine utakua na manufaa endapo utatekelezwa kwa "mfumo wa kina ambao unaweza kushughulikia matatizo makubwa sasa," Rais Recep Tayyip Erdogan amesema katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.

"Mazungumzo ya Istanbul ni hatua muhimu katika juhudi za kidiplomasia wakati ambapo madhara ya vita (Urusi-Ukraine) yanaendelea kuzidi," alisema Erdogan Jumatano, akisisitiza umuhimu wa mazungumzo hayo yanayoandaliwa kupitia jopo la upatanishi la Uturuki ili kumaliza vita vinavyoendelea.

Erdogan alisema kuwa Ankara iko tayari kujadili na Urusi "mapendekezo yoyote yanayoweza kuharakisha kusitishwa kwa mapigano, na kuweka njia ya amani ya haki na ya kudumu."

Alisisitiza kuwa Uturuki inatarajia wadau wote wanaotaka kukomehsa umwagaji damu kati ya Urusi na Ukraine waoneshe msimamo chanya katika mchakato wa amani wa Istanbul.

Juhudi za kidiplomasia za Uturuki

Kwa upande wake, Zelenskyy amesema kuwa Ukraine inatarajia kuanzisha tena mchakato wa kubadilishana wafungwa wa vita na Urusi kufikia mwisho wa mwaka huu.

Aliongeza pia kuwa Ukraine inaamini katika juhudi za kidiplomasia za Uturuki kusaidia kumaliza vita na Urusi.

"Kwa hakika, tulizungumza kwa kina kuhusu hali ya kidiplomasia. Na sasa michakato mingi imeanza kuwa hai zaidi, na tunajitahidi kuhakikisha kwamba shughuli zote zinalenga hasa katika amani," alisema Zelenskyy.

CHANZO:TRT World and Agencies