Erdogan: Uturuki inaendelea kutafuta amani ya kanda licha hofu iliyopo ulimwenguni

Ujazo wa kibiashara na Serbia imefikia Dola Bilioni 3.5, ambapo Uturuki ikilenga shabaha ya kufikia Dola Bilioni 5, amesema rais huyo.

By
Erdogan pia aligusia ukuaji wa uwekezaji wa Uturuki nchini Serbia./Picha:AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa nchi yake itaendelea kuhakikisha kuwa amani na utulivu vinapatikana katika kanda, licha ya hofu iliyopo ulimwenguni kwa sasa, akisisita kuwa Uturuki haitoitekeleza eneo la Balkan.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari pamoja na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic jijini Ankara, Erdogan aligusia jitihada za Uturuki katika kukuza amani na utulivu katika eneo la Balkan.

“Katika kipindi cha ongezeko la hofu duniani, Uturuki inaendelea kufanya jitihada za upatikanaji amani na utulivu katika kanda yetu na kwingineko, na hatujawasahau watu wa Balkan,” alisema.

Hali kadhalika, Erdogan aliangazia ushirikiano wa kiuchumi wa mataifa hayo mawili.

“Ujazo wa kibiashara kati ya Uturuki na Serbia ulifikia Dola Bilioni 3.5 mwaka jana na tumejiwekea lengo la kufika Dola Bilioni 5,” alisema.

Erdogan pia aligusia ukuaji wa uwekezaji wa Uturuki nchini Serbia.

“Wakati makampuni 100 ya nchini Uturuki yakiwa Serbia mwaka 2015, leo hii idadi hiyo imeongezeka na kufikia 1,500 na mtaji wa uwekezaji umefikia Dola Milioni 300,” alisema.

Hali kadhalika, aligusia uhusiano wa kitalii kati ya mataifa hayo mawili.

“Leo hii, Uturuki ni nchi ya pili kutembelewa na Waserbia,” alisema Erdogan.