Uturuki itaadhimisha miaka 10 tangu kutokea kwa jaribio la mapinduzi la Julai 15, 2016.
Madhimisho hayo, yataongozwa na kauli mbiu ya Nia Yetu, Ushindi Wetu, kulingana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Burhanettin Duran.
Maadhimisho hayo yatafanyika katika bustani ya Millet jijini Ankara, siku ya Jumatano, yakihudhuriwa na Rais Recep Tayyip Erdogan.
“Maadhimisho hayo yatahudhuriwa na Rais Recep Tayyip Erdogan, ambapo tutawakumbuka mashahidi wetu kwa sala na shukrani, tukirudia ahadi ya kuwa hakuna atakayekuwa juu ya nia ya taifa,” alisema Duran.
Kupitia chapisho lililowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa NSosyal wa Uturuki, Duran alisema tukio hilo litakukumbuka ujasiri wa umma dhidi ya jaribio hilo lililolenga kutia dosari demokrasia na utawala wa nchi.
Kulingana na Duran, ujasiri wa Julai 15 utaendelea kuishi mioyoni mwa Waturuki.
Jaribio lililoshindwa na mapinduzi hayo, liligharimu maisha ya watu 252 na kujeruhi wengine 2,734, likiongozwa na kiongozi wa FETO, Fethulla Gulen.
Kikundi hicho, kilitumia mwamvuli wa kidini kujipenyeza katika taasisi mbalimbali, ikiwemo Jeshi la Ulinzi la Uturuki, na kujaribu kuchukua madaraka kupitia mapinduzi.
Kabla ya jaribio hilo, kikundi cha FETO kiliendesha operesheni mbalimbali dhidi ya serikali, ikiwemo kumwita aliyekuwa mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (MIT), Hakan Fidan kwa mahojiano.
Kikundi hicho kiliendeleza vuguvugu lake, mara baada ya ushindi wa chama cha AK, kufuatia uchaguzi wa Novemba 1, 2015.
Kiongozi wa kikundi hicho, Fetullah Gulen, alitumia televisheni kutangaza jaribio la mapinduzi hayo.
Jaribio lawekwa wazi
Saa chache kabla ya jaribio hilo, meja wa kijeshi ndani ya jeshi la anga la Uturuki, aliifahamisha MIT, kuwa FETO walikuwa wanajaribu kumuweka kizuizini Fidan.
Taarifa hizo zilimfikia aliyekuwa Kaimu Mnadhimu Mkuu, Jenerali Yasar Guler, ambaye alimfikishia habari Mkuu wa Majeshi, Jenerali Hulusi Akar.
Akar alitoa amri ya ngome ya jeshi la anga kujiimarisha, ikiwemo kufunga anga la kudhibiti shughuli za kijeshi.
Magari ya kijeshi yalisambazwa Ankara, ambako wapinga mapinduzi walikuwa wameyadhibiti.
Sajini taji Bulent Aydin, alikuwa mtu wa kwanza kuuawa katika jaribio hilo, katika makao makuu ya jeshi.
Ndege za F-16 zilionekana zikiruka chini chini jijini Ankara, huku wanajeshi wakifunga daraja la Bosphorus na Msikiti wa Fatih Sultan Mehmet wa jijini Istanbul.
Magaidi wa FETO waliishambulia kwa mabomu Idara ya Operesheni Maalumu ya Polisi Anga na Idara ya Operesheni Maalumu iliyoko Golbasi, Ankara na kushambulia kituo cha MIT, pamoja na kuvamia chombo cha serikali cha TRT, na kuwataka watangazaji kutangaza mapinduzi hayo.
Ilipofika usiku wa Julai 16, Rais Recep Tayyip Erdogan alijitokeza kwenye kituo cha CNN Turk na kuwaomba wananchi kuingia mitaani, na kuiokomboa nchi yao.
Vuguvugu hilo liliendelea mpaka asubuhi, kabla ya waziri mkuu wa wakati huo, Yildirim kutangaza kuwa jaribio hilo kuwa limedhibitiwa.
Kulingana na mamlaka za Uturuki, Gulen ambaye aliasisi taasisi hiyo kwenye miaka ya 1960 na kukimbilia Marekani mwaka 1999, alielekeza mapinduzi ya Julai 15, akiwa jijini Pennsylvania.
Licha ya Uturuki kuwasilisha ombi la kumrudisha Gulen, bado Marekani ilisita kufanya hivyo.
Gulen alifariki dunia Oktoba 20, 2024 katika hospitali ya Mtakatifu Luka jijini Pennsylvania, nchini Marekani.























