Netanyahu: Ziku zimekaribia kwa raia wa Iran kuuangusha utawala wao

Jumla ya raia 555 wa Iran wamepoteza maisha tangu kuanza kwa mashambulizi hayo yanayofanywa kati ya Marekani na Israel.

By
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu./Picha:Wengine

Akizungumza siku ya Jumatatu, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa mashambulizi ya pamoja kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yanalenga kuandaa mazingira mazuri ya raia wa Iran kuuondoa madarakani utawala wao.

"Siku hiyo ipo karibu. Na siku hiyo ikifika, Israel na Marekani zitakuwa pamoja na raia wa Iran,"alisema Netanyahu.

Netanyahu amesisitiza kuwa ni wakati muafaka kwa raia wa Iran kuuondoa utawala uliopo madarakani kwa sasa, huku Rais Donald Trump wa Marekani akiwataka Wairan kuichukua nchi yao.

Jumla ya raia 555 wa Iran wamepoteza maisha tangu kuanza kwa mashambulizi hayo yanayofanywa pamoja na Marekani na Israel.