| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Viongozi kadhaa wa Afrika wameipongeza timu ya Arsenal kwa kushinda ubingwa wa EPL
Marais wa Kenya, Rwanda na Zimbabwe wameipongeza Arsenal kutwaa ubingwa wa EPL.
Viongozi kadhaa wa Afrika wameipongeza timu ya Arsenal kwa kushinda ubingwa wa EPL
Mara ya mwisho Arsenal kushinda ubingwa huo ilikuwa chini ya kocha Arsene Wenger zaidi ya miaka 20 iliopita. Picha:@Arsenal / x

Rais William Ruto wa Kenya ameungana na mamilioni ya mashabiki wa Arsenal F.C. duniani kusherehekea ubingwa wa EPL 2025/26 baada ya klabu hiyo kutwaa taji hilo.

Mara ya mwisho Arsenal kushinda ubingwa huo ilikuwa chini ya kocha Arsene Wenger zaidi ya miaka 20 iliopita.

Ruto amesema safari ya timu hiyo kutoka nyakati ngumu hadi kuwa mabingwa imeonsha ari ya matumaini, uvumilivu na bidii.

Kupitia ujumbe wake katika mitandao ya kijamii, Ruto alisema ushindi huo umeidhihirishia dunia kuwa nidhamu, mshikamano na kujituma huleta mafanikio.

Naye Rais wa Rwanda Paul Kagame ameipongeza klabu ya Arsenal F.C. baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL) msimu huu.

Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa X, Kagame alisema: “Hongereni Arsenal, washirika wetu wa 'VisitRwanda', kwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England baada ya msimu mgumu uliokuwa na ushindani! Ubingwa unaostahili kabisa!”

Katika ujumbe wake, Kagame alisema ushindi huo ni matokeo ya juhudi kubwa, mshikamano na ushindani mkali uliodumu kwa msimu mzima, akisisitiza kuwa klabu hiyo imeonesha nidhamu na bidii iliyoiwezesha kufikia mafanikio hayo makubwa.

Arsenal imekuwa na uhusiano wa kibiashara na Rwanda kupitia mpango wa kutangaza utalii wa 'VisitRwanda', ambao umeiweka klabu hiyo karibu zaidi na taifa hilo katika masuala ya matangazo na kuimarisha ya utalii.

Rais Hakainde Hichilema wa Zambia ameungana na viongozi wengine Afrika kuipongeza Arsenal F.C. baada ya klabu hiyo kutwaa ubingwa wa EPL.

Katika ujumbe wake, alisema kuwa ingawa kuna mambo muhimu ya kisiasa ambayo hawakubaliani, aliona ni vyema kuwatambua wapinzani na kuwapongeza mashabiki wa Arsenal.

“Hata kama hatukubaliani kabisa kuhusu suala moja muhimu sana, katika wiki hii yenye shughuli nyingi za kisiasa, naomba kwa muda niwapongeze wapinzani… Hongereni mashabiki wote wa Arsenal,” alisema Hichilema.

CHANZO:TRT Afrika