| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Mhudumu wa Shirika la Ndege la KLM akutwa na virusi vya hanta
Kulingana na Shirika la Habari la RTL, mhudumu huyo wa ndege, anadaiwa kukutana na raia wa Kiholanzi aliyeshuka kutoka ndege ya KLM na baadaye kufariki dunia kwa ugonjwa wa hanta akiwa Afrika Kusini.
Mhudumu wa Shirika la Ndege la KLM akutwa na virusi vya hanta
Kulingana na chombo cha habari cha RTL, mfanyakazi huyo wa ndege, anadaiwa kukutana na raia wa Kiholanzi aliyeshuka kutoka ndege ya KLM./Picha:Wengine

Mhudumu wa Shirika la Ndege la Uholanzi (KLM) amepimwa na kugundulika kupatikana na virusi vya hanta.

Kulingana na msemaji wa wizara ya afya ya Uholanzi, kwa sasa, mfanyakazi huyo anapokea matibabu katika hospitali moja jijini Amsterdam.

“Mgonjwa huyo anapokea matibabu baada ya vipimo kuonesha kuwa ameambukizwa virusi hivyo,” alisema Mischa Stubenitsky.

Kulingana na chombo cha habari cha RTL, mfanyakazi huyo wa ndege, anadaiwa kukutana na raia wa Kiholanzi aliyeshuka kutoka ndege ya KLM na baadaye kufariki dunia kwa ugonjwa wa hanta akiwa Afrika Kusini.

Shirika la Ndege la KLM, lilisema siku ya Jumatano kuwa, abiria huyo alikuwa ndani ya ndege hiyo katika safari ya kutoka Johannesburg kuelekea Uholanzi, lakini alishushwa kutoka kwenye ndege hiyo, muda mfupi kabla ya kuruka.

"Kutokana na hali yake ya kiafya, wahudumu wetu wa ndege waliona haitokuwa busara kwa abiria yule kuendelea na safari,” taarifa ya KLM imeeleza.

CHANZO:AFP