Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amepata mapokezi makubwa kutoka kwa mwenyeji wake Kassym-Jomart Tokayev mara baada ya kuwasili nchini Kazakhstan, siku ya Alhamisi.
Msafara wa Erdogan ulipokelewa kwa shamrashamra kubwa, zilizonakshiwa na bendera za mataifa hayo mawili, kabla ya kuelekea kwenye Jumba la Uhuru jijini Astana.
Mara baada ya kuwasili kwake, nyimbo za taifa za nchi hizo zilipigwa, na muda mfupi baadaye Rais Erdogan akakagua gwaride la heshima.
Kisha, viongozi hao wakapata picha ya pamoja na kisha na kuendelea na mazungumzo yao ya ana kwa ana.
Baadaye siku hiyo, Erdogan anatarajiwa kuwa mwenyekiti mwenza wa kikao cha sita kati ya Uturuki na Kazakhstan.
Viongozi hao wanatarajia kusaini mikataba ya nchi hizo mbili pamoja na kufanya mkutano wa pamoja na wanahabari.
Viongozi mbalimbali wa Uturuki walihudhuria shughuli hiyo, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan, Waziri wa Ulinzi Yasar Guler, Waziri wa Biashara Omer Bolat na Mkuruenzi wa Mawasiliano ya Rais Burhanettin Duran.


















