Rais wa Tunisia Kais Saied amemfuta kazi Waziri wa Nishati Fatma Thabet siku ya Jumanne, huku kukiwa wasiwasi kuhusu miradi ya nishati endelevu ambayo inatarajiwa kupigiwa kura bungeni.
Saied anasema amemteua Waziri wa Makazi na Miundombinu Salah Eddine Zouari kusimamia wizara hiyo kwa muda. Hakukuwa na maelezo zaidi kuhusu uamuzi huo.
Hatua hii inakuja huku serikali ya Saied ikitaka kupitisha sheria kuhusu nishati enedelevu, ambazo zinatarajiwa kupigiwa kura baadaye Jumanne.
Umuhimuwa nishati safi
Miradi hiyo ni sehemu ya juhudi za Tunisia kuimarisha uzalishaji wa nishati safi. Baadhi ya wabunge na vyama vya kisiasa wanapinga miradi hiyo, wakiieleza kama aina ya "ukoloni wa nishati."
Wameshtumu kutengwa kwa shirika la umeme la taifa (STEG) kwenye kandarasi, ambayo wanasema ilipewa makampuni ya nje.
Fatma Thabet aliteuliwa Waziri wa Viwanda, Nishati, na Madini Januari 24 2024.
Awali alikuwa Waziri wa Viwanda na Waziri wa Fedha, ikiwemo Mkuu wa Masuala ya Uchumi.
Alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ukarabati wa Viwanda katika Wizara ya Viwanda na kuwa mwakilishi wa Serikali katika Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ya Tunisia na Imarati.

















