| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Julai 15 ilimaliza historia ya mapinduzi ya kijeshi nchini Uturuki: Spika wa Bunge
Numan Kurtulmus anasema kuwa upkaidi dhidi ya jaribio la mapinduzi la mwaka 2016 uliashiria 'ushindi wa demokrasia' na 'matakwa ya taifa'.
Julai 15 ilimaliza historia ya mapinduzi ya kijeshi nchini Uturuki: Spika wa Bunge
Kurtulmus alisema uongozi wa kisiasa, bunge, umma, misikiti na vyombo vya habari vilichukua nafasi muhimu katika kulishinda jaribio la mapinduzi. / / AA

Wananchi wa Uturuki walihitimisha historia ndefu ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo kupitia upinzani wao dhidi ya jaribio la mapinduzi lililoshindwa la tarehe 15 Julai 2016, alisema Spika wa Bunge Numan Kurtulmus.

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Demokrasia na Umoja wa Kitaifa iliyofanyika katika Bunge siku ya Jumatano, Kurtulmuş alisema urithi mkubwa wa usiku huo ulikuwa “ushindi wa demokrasia” na “matakwa ya taifa.”

Alisema Uturuki imepitia mfululizo wa mapinduzi ya kijeshi yaliyoanzia mwishoni mwa kipindi cha Dola ya Ottoman na kuendelea katika historia ya jamhuri hiyo pamoja na mfumo wake wa siasa za vyama vingi.

“Wananchi waliamua hatima ya nchi yao asubuhi ya Julai 15 na waliondoa kabisa mienendo wa mapinduzi ya kijeshi kwenye historia,” alisema.

Kurtulmuş alisema uongozi wa kisiasa, Bunge, wananchi, misikiti na vyombo vya habari vilikuwa na nafasi muhimu katika kushinda jaribio hilo la mapinduzi.

Aliashiria wito wa Rais Recep Tayyip Erdogan kupitia televisheni uliowataka wananchi kujitokeza mitaani, akisema ujumbe huo uliwahamasisha mamilioni ya watu kupinga waliokuwa wakijaribu kupindua serikali.

Pia aliwasifu wabunge kutoka pande mbalimbali za kisiasa waliokusanyika ndani ya Bunge wakati jengo hilo lilipokuwa likishambuliwa, akisema uwepo wao ulionyesha nguvu ya demokrasia na umoja wa kitaifa.

Alisema matukio hayo yalionyesha umuhimu wa kuhakikisha taasisi za serikali haziwi eneo la ushawishi wa kundi lolote, huku akisisitiza umuhimu wa uwazi, taasisi imara, utawala wa sheria na mshikamano wa kitaifa.

Mnamo Julai 15, 2016, sehemu la kundi ndani ya Jeshi la Uturuki lililohusishwa na Shirika la Kigaidi la Fethullah (FETO) lilijaribu kupindua serikali iliyochaguliwa kidemokrasia nchini humo.

Waliopanga mapinduzi hayo walishambulia kwa mabomu Bunge na taasisi nyingine za serikali, na kuwafyatulia risasi raia, na kusababisha vifo vya watu 253 huku maelfu wengine wakijeruhiwa.

CHANZO:AA
Soma zaidi
Rais Erdogan wa Uturuki kukutana na Abbas jijini Ankara kujadili hali ya Palestina
Katika picha: Vivutio mbalimbali vya Uturuki vyang’aa mwanga kushangilia mkataba wa Ulinzi wa Mecca
Rais Erdogan wa Uturuki akutana Kansela Stocker wa Austria
Ndege ya Bayraktar TB2 ya Uturuki yasaidia kudhibiti moto wa nyika nchini Albania
Makubaliano ya Makka ni ya ulinzi wa pamoja lakini hayalengi shabaha au adui yeyote: Waziri Fidan
Uturuki yaadhimisha kumbukumbu ya miaka 59 ya ASEAN na kuahidi kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
Uturuki yakanusha madai kuwa Mkataba wa Ulinzi wa Makkah unakinzana na Kifungu cha 5 cha NATO
Mkataba wa Makkah uko wazi kwa mataifa mengine rafiki: Rais Erdogan wa Uturuki
Ukimshambulia mmoja wetu umetushambulia sote, Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan wasema
Erdogan kufanya ziara Saudi Arabia atakutana na MBS na Waziri Mkuu wa Pakistan
Mashambulizi ya Israel yanatishia usalama wa Syria: Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki
Muswada wa “Uturuki Isiyo na Ugaidi” wafungua hatua muhimu katika kukomesha ugaidi: Erdogan
Mkuu wa mawasiliano wa Uturuki anasema Israel inahujumu juhudi za amani za Gaza
Uturuki inaweka historia kwa kusafirisha treni ya kwanza iliyotengenezwa nchini humo kwenda Afrika
Mkuu wa shirika la ujasusi wa Uturuki akutana na kiongozi wa Hamas kujadili mpango wa amani wa Gaza
Rais wa Uturuki na Mwana Mfalme wa Saudia wajadili usalama wa kikanda na mpango wa amani wa Gaza
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki na Kuwait wajadili yanayojiri katika kanda
Mkuu wa mawasiliano wa Uturuki anasema Israel inahujumu juhudi za kutafuta amani Gaza
Uturuki yalaani mashambulizi ya Israel huko Gaza, ikimtuhumu Netanyahu kwa kuhujumu juhudi za amani
Mpango wa 'Uturuki Isiyo na Ugaidi' kupata msukumo kupitia hatua za bunge: Erdogan