Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Romania, Mircea Lucescu amefariki dunia.
Kocha huyo, mwenye umri wa miaka 80, amefariki dunia Aprili 7, 2026 kwa maradhi ya moyo, ikiwa ni siku chache baada kujiuzulu kwa sababu za kiafya.
Lucescu, ambaye pia amewahi kuwika na klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki, amefariki siku chache baada ya Romania kushindwa kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia, baada ya kufungwa 1-0 na Uturuki.
Mzaliwa wa jijini Bucharest, Lucescu amewahi pia kuzifudisha klabu zingine za Ulaya, ikiwemo Inter Milan na Shakhtar Donetsk, katika miaka yake 47 ya kufundisha soka barani Ulaya.
Alikuwa kocha wa tano barani Ulaya kuongoza timu katika michezo 100 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, akiivuka rekodi hiyo mwaka 2015.
Rekodi hiyo inamuweka kundi moja na makocha wengine wakubwa, akiwemo Sir Alex Ferguson, Carlo Ancelotti, Arsene Wenger na Jose Mourinho.














